Ugonjwa Usiojulikana waua watu 27 Congo
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza jana December 05,2024 kuwa iko katika tahadhari ya juu kutokana na kuzuka kwa ugonjwa usiojulikana ambao umesababisha vifo vya Watu kadhaa ndani ya muda wa zaidi ya mwezi mmoja.
Mtandao wa DW Kiswahili umeripoti kuwa Waziri wa Afya wa Nchi hiyo, Samuel Roger Kamba amewaambia Waandishi wa Habari Mjini Kinshasa kuwa Mamlaka iko macho na kwamba wanafuatilia mlipuko wa ugonjwa huo kwa ukaribu sana.
Waziri huyo amesema jana kuwa wamehesabu miili ya Watu 27 katika vituo vya afya waliofariki kutokana na ugonjwa huo ambao unasababisha dalili zinazofanana na mafua makali ambazo ni homa, kikohozi na maumivu ya kichwa.
Ugonjwa huo uligunduliwa kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi October mwaka huu na hadi sasa umeripotiwa zaidi katika eneo la Panzi, takriban kilomita 700 kusini mashariki mwa mji mkuu Kinshasa.
Kamba amesema Watu wengine 44 wameripotiwa kufariki pia lakini ameweka bayana kuwa huenda vifo hivyo vimetokana na sababu nyingine.
Wagonjwa zaidi ya 23,000 wamepatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa mkoa wa Njombe
Wagonjwa zaidi ya 23,000 wamepatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa mkoa wa Njombe huku wagonjwa wa dharura na mahututi wakiwa 1,322 katika kipindi cha mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu.
Hayo yameelezwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufani mkoa wa Njombe Dk. Gilbert Kwesi katika uzinduzi wa huduma ya uchunguzi wa magonjwa ya mfumo wa chakula (ENDOSCOPY UNIT) uliofanyika katika hospitali hiyo.
Dk. Kwesi amesema magonjwa hayo ya mfumo wa chakula mchanganyiko yamekuwa yakiongoza kwa kuwa na idadi ya wagonjwa wengi ambapo kwa kipindi cha Januari hadi Septemba wagonjwa 566 wamefanyiwa uchunguzi na kutibiwa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka mara baada ya kuzindua huduma hiyo amewataka watumishi wa hospitali kuendelea kutoa huduma bora sambamba na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.
“Fanyeni kazi kwa kuzingatia maadili lakini tembeeni kifua mbele kwa sababu serikali inaendelea kuhakikisha mnafanya kazi katika mazingira rafiki na kuridhisha pamoja na kutatua matatizo yenu ya kimaslahi,” amesema Mtaka.
Katibu Tawala Mkoa wa Njombe,Judica Omary ametoa rai kwa watoa huduma hao kuongeza ufanisi ili maboresho ya vifaa tiba yaweze kuleta tija.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Kissa Kasongwa ametoa wito kwa wakazi wa Njombe kuiamini hospitali ya rufaa ya mkoa huo kutokana na uwapo wa vifaa tiba vya kibingwa vya teknolojia ya kisasa na huduma zake zikiwa ni bora.
Kuzinduliwa kwa huduma ya tiba kwa wenye matatizo katika mfumo wa chakula kunaifanya hospitali ya rufaa Mkoa wa Njombe kuwa na huduma zote muhimu ambazo awali wakazi wa mkoa huo walilazimika kuzifuata katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Maambukizi ya Marburg yapungua nchini Rwanda
MAAMBUKIZI ya virusi vya ugonjwa wa Marburg nchini Rwanda yamepungua baada ya watu waliokuwa hatarini kuanza kupatiwa chanjo.
Waziri wa afya nchini Rwanda Sabin Nsanzimana amesema tangu serikali kwa kushirikiana na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Afrika CDC kutoa chanjo maambukizi ya ugonjwa huo yamepungua katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.
#SOMA ZAIDI HAPA🔗🔥; Kuhusu Ugonjwa wa Marburg,chanzo,dalili
Hatahivyo,Mkuu wa Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Afrika CDC Jean Kaseya amesema licha ya kupungua kwa maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Marburg kwa sasa wanakabiliana na tatizo la Mpox ambalo limeshafika katika nchi sita Barani Afrika.
Maambukizi Ya Malaria Yapungua Hadi Asilimia 8.1 Kwa Mwaka 2015-2022
Wizara ya afya kupitia mpango wa taifa wa kudhibiti malaria kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI imepunguza kiwango cha malaria kwa asilimia 45 kutoka 14.8 ya mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 8.1 mwaka 2022.
Hayo yamebainishwa na Naibu waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge na Masuala ya Ukimwi kilichofanyika katika ukumbi wa bunge Jijini Dodoma.
Dkt. Mollel amesema kuwa, Serikali imetekeleza mikakati ya udhibiti wa mbu waenezao Malaria kwa njia ya utengamano pamoja na ugunduzi, matibabu na tiba kinga dhidi ya malaria ambapo imewezesha mafanikio hayo kwa takribani miaka 8 na kupunguza wagonjwa wa malaria wanaotibiwa kama wagonjwa wa nje (OPD) kwa asilimia 55.
“Serikali imetekeleza afua mbali mbali kwa takriban miaka minane na kufanikiwa kupunguza kiwango cha malaria kwa asilimia 45 kutoka 14.8 hadi 8.1 pamoja na kupunguza wagonjwa wa nje kwa asilimia 55 ambapo awali walikua ni milioni 7.7 hadi 3.5 kwa mwaka 2023”. Amesema Dkt. Mollel
Aidha, Dkt. Mollel amesema kuwa kwa sasa mpango wa taifa wa kudhibiti malaria unatekeleza mpango mkakati wa sita wa mwaka 2021 mpaka 2025 wenye lengo la kupunguza kiwango cha chini kutoka asilimia 7.5 (2017) hadi 3.5 ifikapo 2025
Kwa Upande wake Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Bi Bernadeta Mushashu ameishauri serikali kuongeza afua za kutokomeza malaria katika mikoa iliyo katika hatari ya maambukiza ya malaria kama vile Tabora unaoongoza kwa asilimia 23.4, Mtwara kwa asilimia 20, Kagera asilimia 18, Shinyanga 16%na Mara 15%.
Aidha ameipongeza Serikali kwa juhudi na malengo ya kuendelea kutekeleza afua za kutokomeza malaria pamoja na kufanikiwa kupunguza mpaka chini ya asilimia katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Dodoma, Singida, Iringa, Songwe, Dar es Salaam na Mwanza.
Hata hivyo wametoa rai kwa wananchi kuendelea kutekeleza ushauri wa madaktari kuhusu matumizi sahihi ya vyandarua pamoja na kuweka mazingira yanayotuzunguka safi na salama ili kuzuia mazalia ya viluilui ya mbu.
Watu 41 wamethibitishwa kuugua ugonjwa wa Marburg Rwanda
Marekani yawaonya raia wake kufikiria upya safari ya kuelekea Rwanda,kisa kusambaa kwa Marburg
Marekani siku ya Jumatatu imewaonya raia wake kwamba wanapaswa kufikiria upya kusafiri kwenda Rwanda, ikitaja mlipuko wa virusi hatari vya Marburg.
Taifa hilo la Afrika Mashariki mwishoni mwa juma lilisema ugonjwa huo unaofanana na Ebola umeua watu 12, wengi wao wakiwa wahudumu wa afya, tangu mlipuko huo ulipotangazwa mwishoni mwa mwezi uliopita.
Ushauri wa kusafiri kwenda Rwanda umepandishwa hadi kiwango cha tatu, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema, ikimaanisha kwamba Wamarekani “wanapaswa kufikiria upya kusafiri kwenda Rwanda.”
Kiwango hicho kimeshika nafasi ya 4, ambayo inawatahadharisha raia kutosafiri hata nchi.
Kulingana na wizara ya afya ya Rwanda, watu 41 wamethibitishwa kuugua ugonjwa huo.
Bodi ya Maendeleo ya Rwanda ilisema hatua za usafiri zilikuwa zimewekwa Jumapili.
Ilisema ukaguzi wa halijoto, dodoso za abiria na vituo vya kusafisha mikono vitaletwa katika sehemu za kuondoka, na kuwataka wasafiri kujifuatilia wenyewe kwa dalili kama vile homa.
Marburg huambukizwa kwa wanadamu kutoka kwa popo wa matunda, na ni sehemu ya familia inayoitwa filovirus ambayo pia inajumuisha Ebola.
#SOMA zaidi hapa Ugonjwa huu; https://www.afyaclass.com/2024/10/ugonjwa-wa-marburgchanzo-na-dalili-zake.html?m=1
Nchi ya Rwanda kuanza majaribio ya chanjo na Tiba dhidi ya Ugonjwa wa Marburg
Nchi ya Rwanda iko tayari kuanza majaribio ya chanjo na matibabu ya ugonjwa wa Marburg, Yvan Butera, waziri msaidizi wa afya alisema siku ya Alhamisi, huku taifa hilo la Afrika Mashariki likipambana na mlipuko wake wa kwanza wa homa hay ya virusi ambayo imewaua watu11.
“Hii ni sehemu ya juhudi zetu za kusaidia watu kupona haraka kwa kutumia chanjo na dawa zilizotengenezwa mahsusi kupambana na mlipuko huu, kwa sasa katika awamu ya mwisho ya utafiti,” waziri, Sabin Nsanzimana, aliiambia Reuters.
“Tunashirikiana na makampuni ya dawa yaliyotengeneza dawa hizi, pamoja na Shirika la Afya Ulimwenguni ili kuharakisha mchakato huo kupitia ushirikiano wa kimataifa.”
Alisema serikali inazungumza na makampuni yaliyoko Marekani na Ulaya.
Wizara hiyo ilikuwa ikifuatilia watu 410 ambao walikuwa wamewasiliana na wale walioambukizwa, aliongeza, huku i wengine watano waliopimwa wakibainika kuwa hawana, lakini walisubiri matokeo ya vipimo zaidi
Ugonjwa huo ulithibitishwa kwa mara ya kwanza mwishoni mwa Septemba, na watu 36 wameripotiwa kupata maradhi hayo hadi sasa, data ya wizara ya afya inaonyesha.