DALILI ZA UGONJWA WA AKILI(PSYCHOSIS),CHANZO NA TIBA
Kama una mojawapo ya dalili zifuatazo basi unaweza ukawa na ugonjwa wa akili,ukichaa (pyschosis) na unahitaji matibabu
1)Kusikia sauti zinakusemesha na kua kama upo kwenye mdahalo na watu ambao huawoni (Auditory hallucinations (eg, hearing voices)
2) Kua na hisia,kuishi kwa wasiwasi kwa kudhani unafuatiliwa na watu au vikundi vya kihalifu (Persecutory delusions or paranoid delusions (eg, believing one is being followed and harassed by gangs)
3)Kuhisi kwamba mawazo yako yanaongozwa na mtu mwingine (Delusions of control (eg, believing one’s thoughts or actions are being controlled by other persons or objects)
4) Kuhisi kwamba kwenye pua zako kuna minyoo nk (Somatic delusions (eg, believing one’s sinuses have been infested by worms)
5)Kuhisi na kujiona na kutangaza kwamba unadate na mwigizaji maarufu wa filamu (Erotomanic delusions (eg, believing a famous movie star is in love with them)
6)Kujiona kua wewe ndio tajiri na una mali na unamiliki kila kitu duniani (Grandiose delusions (eg, believing one is a billionaire CEO who owns casinos around the world)
MAGONJWA YA AKILI,DALILI,CHANZO NA TIBA YAKE
Matatizo ya akili kwa asilimia kubwa huhusisha ubongo wa mtu,mood,uwezo wake wa kihisia,uwezo wake wa kufikiria,tabia yake pamoja na uwezo wake wa kufanya maamumizi sahihi.
matatizo ya akili/magonjwa ya akili kwa kitaalam mental disorders or mental diseases yapo mengi,na hapa chini ni orodha ya baadhi ya matatizo hayo ya akili;
1. Depression
2. Anxiety
3. Obsessive-Compulsive disorder(OCD)
4. Bipolar disorder
5. Post traumatic stress disorder(PTSD)
6. Schizophrenia
7. Personality disoder N.k
DALILI ZA MAGONJWA YA AKILI KWA UJUMLA WAKE NI PAMOJA NA;
- Mtu kuwa na huzuni isioisha,kusononeka na kuhisi kupoteza kabsa tumaini
- Mtu kuongezeka uzito sana au kupungua uzito kwa kasi sana
- Mtu kulala sana kupita kawaida au mtu kukosa kabsa usingizi wakati wa usiku
- Mwili kuchoka kupita kawaida
- Mtu kujiona mkosaji na mwenye hatia kila mara,mpaka kwenye vitu ambavyo kwa hali ya kawaida sio kosa kuvifanya
- Mtu kupoteza kumbu kumbu na kusahau vitu mara kwa mara
- Mtu kufikiria kila mara kuhusu kifo na kutaka kujitoa mhanga mwenyewe
- Mtu kuonyesha dalili za kuchanganyikiwa au kuona na kuongea na vitu ambavyo kwa hali yakawaida haviongei au havionekani
- Mtu kufanya kitu hicho hicho muda wote yaani kwa kurudia rudia au kufanya kitu kimoja kwa muda mrefu kuliko kawaida mfano kufanya usafi n.k
- Mtu kuongea sana kupita kawaida
- Mtu kufanya kazi sana kupita kawaida yake
- Mtu kuwaza vitu kwa haraka haraka yaani racing thoughts
- Mtu kuwa mchafu kuliko kawaida
- Mtu kuwa na wasi wasi sana au hofu kuu kwenye mambo yakawaida tu
- Mtu kupatwa na maumivu ya tumbo,maumivu ya kifua,kifua kuwa kizito sana,mapigo ya moyo kwenda mbio sana mara kwa mara,maumivu ya kichwa sana,kizunguzungu kikali, Dalili Zote hizi hutokea sana hasa kwa mtu mwenye shida ya Anxiety
- Mtu kuwa mgumu wa kuelewa maelekezo yakawaida kabsa n.k
CHANZO CHA MATATIZO HAYA YA AKILI KWA UJUMLA WAKE NI PAMOJA NA;
• Mtu kurithi vinasaba au genes za matatizo ya akili kutoka kwenye Familia yake
• Matatizo ya kimazingira
• Shida ya Chemical Imbalance kwenye Ubongo
• Matumizi ya madawa mbali mbali ya kulevyia
• Maambukizi ya Magonjwa mbali mbali
• Matumizi ya baadhi ya dawa kimakosa
• Mtu kudondoka,kupata ajali na kuumia au kugonga maeneo ya kichwani yaani Head Trauma
• Mtu kuwa na tatizo la Msongo wa mawazo kwa muda mrefu bila kupata tiba
• Mtu kukosa support kutoka kwa watu wake wakaribu kwenye kila aina ya mahitaji yake muhimu yaani low social support n.k
MATIBABU YA MAGONJWA HAYA YA AKILI,
- Kwa asilimia kubwa matibabu ya magonjwa haya ya akili hutegemea na chanzo chake,Ila kwa ujumla wake matibabu hayo ni pamoja na;
✓ Matumizi ya dawa jamii ya Antidepressants
✓ Matumizi ya dawa jamii ya anti-anxiety
✓ Matumizi ya dawa jamii ya Antipsychotic
✓ Matumizi ya Lithium n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.