TATIZO LA MTOTO KUZALIWA BILA SEHEMU YA HAJA KUBWA,CHANZO,DALILI NA TIBA
Tatizo hili huweza kutokea kwa baadhi ya watoto,na tafiti zinaonyesha kwamba,tatizo hili hutokea kwa watoto wa jinsia ya kiume zaidi kuliko ya kike,
Na mara nyingi likitokea kwa watoto wa kike huwa,Rectum,bladder pamoja na uke hutengeneza tundu moja ambalo kwa kitaalam hujulikana kama cloaca.
CHANZO CHA TATIZO LA MTOTO KUZALIWA BILA SEHEMU YA HAJA KUBWA
• Tatizo hili hutokea mtoto akiwa tumboni hasa ujauzito ukiwa na wiki tano mpaka saba, na chanzo halisi cha tatizo hili bado hakijulikani,
Na mara nyingi watoto ambao huzaliwa na tatizo hili wanakuwa na shida nyingine kwenye rectum.
DALILI ZA TATIZO LA MTOTO KUZALIWA BILA SEHEMU YA HAJA KUBWA
Kwa asilimia kubwa dalili za tatizo hili huanza kuonekana mara tu baada ya mtoto kuzaliwa, na dalili hizo ni kama vile;
- Mtoto kutokuwa na tundu la haja kubwa(no anal opening)
- Tundu la haja kubwa kuwepo sehemu ambayo sio sahihi,mfano karibu kabsa na ukeni n.k
- Mtoto kutojisaidia haja kubwa kuanzia masaa 24 mpaka 48 toka azaliwe
- Haja kubwa kutokea sehemu ambayo sio sahihi mfano kwenye uke,urethra,chini ya uume,kwenye scrotum n.k
- Tumbo la mtoto kuvimba
- Na asilimia kubwa ya watoto wenye tatizo hili la kukosa sehemu ya haja kubwa huwa na matatizo mengine kama vile;
• Kuwepo kwa tundu kati ya Rectum pamoja na via vyao vya uzazi au njia ya mkojo
• Defects kwenye njia ya mkojo pamoja na Figo
• Shida kwenye uti wa mgongo
• Shida kwenye mikono na miguu
• Shida ya tracheal au windpipe
• Shida kwenye esophageal
• Tatizo la Down syndrome(chromosomal condition),tatizo ambalo huweza kuhusisha hatua za ukuaji wa mtoto kuchelewa kama vile: cognitive delay, intellectual disability, a characteristic facial appearance, pamoja na misuli kuwa dhaifu sana.
• Ugonjwa wa Hirschsprung, ambao huhusisha kukosekana kwa Nerve cells kwenye utumbo mkubwa
• Tatizo la duodenal atresia,ambapo huhusisha defects kwenye sehemu ya kwanza ya Small bowel.
• Matatizo ya moyo(congenital heart defects) N.k.
TATIZO LA MTOTO KUZALIWA BILA SEHEMU YA HAJA KUBWA HUGUNDULIKAJE?
Tatizo hili kwa asilimia kubwa hugundulika mara tu baada ya mtoto kuzaliwa,
- Kuanza kuonekana kwa dalili zote ambazo nimeeleza hapo juu, pamoja na;
- kufanya physical examination(kumkagua mtoto baada ya kuzaliwa)
- Pia vipimo vingine huweza kufanyika ili kujua ukubwa wa tatizo pamoja na madhara yake, kama vile;
• Kufanya X-ray ya tumboni huweza kusaidia pia kujua ukubwa wa tatizo hili
• X-ray ya uti wa mgongo kuangalia defects zozote kwenye uti wa mgongo
• Kipimo cha echocardiogram kuangalia shida yoyote kwenye moyo
• Kipimo cha MRI Kuangalia shida yoyote kwenye esophageal,uwepo wa tundu kwenye trachea n.k
MATIBABU YA TATIZO LA MTOTO KUZALIWA BILA SEHEMU YA HAJA KUBWA
Tatizo hili huhitaji matibabu ya haraka kwa mtoto, na asilimia kubwa ya watoto hufanyiwa upasuaji wa kurekebisha sehemu hii.
- Pia huduma ya temporary colostomy inaweza kumsaidia mtoto kukuwa kuwa kabla ya upasuaji,
Pia utaelekezwa jinsi ya kumfanyia mtoto wako huduma ya Anal dilation, ili kusaidia tundu la haja kubwa kutokuwa dogo zaidi,ambapo utafanya zoezi hili kwa miezi kadhaa.