Athari za kuzuia kupiga chafya au Madhara ya Kuzuia kupiga chafya,Soma Hapa kufahamu
Watu wengi hawana elimu hii, hawafahamu kwamba kupiga chafya ni afya na hutakiwi kuzuia kupiga chafya, Ingawa linaweza kuwa tatizo pia linalohitaji tiba kabsa kwa baadhi ya Watu,
Madaktari wanaonya kuzuia kupiga chafya kunaweza kuwa na athari. Unaweza kupata madhara makubwa hata kufikia hatua ya kupasuka Koo n.k
Mfano ni kwa Mwanaume mmoja; Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 30 alilazwa katika Hospitali ya Ninewells huko Dundee, Uingereza, akiwa na maumivu makali ya shingo.
Chanzo cha shida hii ni kwamba; Alipopiga chafya, alifunika pua na mdomo kwa mikono yake.
Kwa kuzuia chafya hiyo, koo lake lilipanuka hadi kuwa na upana wa milimita 2, Hii Ilibainika kupitia uchunguzi na Pia alionekana ana jeraha kooni.
Fahamu kwamba kufunika mdomo na pua wakati mtu anapiga chafya huongeza kanieneo kwenye njia ya juu ya hewa kwa mara 20.
Athari za kuzuia kupiga chafya au Madhara ya Kuzuia kupiga chafya
Zipo athari au Madhara mbali mbali ya Kuzuia kupiga chafya,Athari hizo ni pamoja na;
- kuna hatari ya sikio kupasuka kutokana na kani kuwa kubwa.
- Pia, unaweza kupata maambukizi ya mishipa ya damu
- Vile vile mifupa ya kifua inaweza kuvunjika
- au majeraha mengine makubwa yanaweza kutokea.
Katika uchunguzi wa mtu aliyepata majeraha, madaktari wanasema sauti ilikuwa ikitoka kooni na mtu huyo alishindwa kuizuia. Wakati wa kupiga chafya, mtu huyo alikuwa akiendesha gari akiwa amejifunga mkanda kwa mujibu wa madaktari.
Tukio sawa na hilo lilitokea 2018 huko Uingereza. Mwanaume mmoja huko Leicester alipata majera ya koo baada ya kuzuia chafya. Alipata maumivu makali kwenye koo lake, kiasi cha kushindwa kuongea na kumeza chakula.
Matokeo yake, madaktari walimlisha kupitia bomba kwa siku saba.
Faida za Kupiga Chafya ni Zipi kwako?
”kupiga chafya ni utaratibu wa asili na ni mchakato wa ulinzi wa mwili wa binadamu.”
Fahamu,kupiga chafya huzuia kitu chochote chenye muwasho kuingia mwilini kupitia puani, na hivyo mtu hapaswi kamwe kuacha kupiga chafya.
“Wakati wa kupiga chafya, maambukizi yanayowasha kama vile virusi hutolewa kutoka puani pamoja na mate na kamasi,
Tunapaswa kufunika pua zetu kwa mikono yetu ili kuzuia virusi kuenea kwa wale walio karibu nasi lakini tusizuie kupiga chafya,”
Kuacha kupiga chafya kunaweza kusababisha majera ya koo. Ingawa matukio kama hayo ni nadra, lakini wakati mwingine yanaweza kuwa hatari.
Sababu za Kupiga Chafya ni zipi?
kupiga chafya kunaweza kusababishwa na sababu mbali mbali ikiwemo; vijidudu kama bacteria, virusi au vumbi. Wakati mwingine hata mionzi yenye nguvu ya jua inaweza kusababisha kupiga chafya.
Utafiti: Uchunguzi kwa watu zaidi ya 1,000, nchini Ujerumani uliripoti kuwa miale mikali au mwanga mkali wa jua husababisha kupiga chafya.
Wataalamu wengine wanaamini sababu ya kupiga chafya inaweza kuwa ya urithi. Na baadhi ya Watu huripoti kupiga chafya baada ya kula chakula kingi.
Chafya ya mtu inaweza kufikia mita nane au futi 26.
Utafiti uliofanywa na Lydia Boroiba katika Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts uligundua chembechembe zinazotolewa kutoka puani wakati wa kupiga chafya zinaweza kuelea hewani kwa dakika kadhaa.