Sababu za kupumzika kitandani au kuanza Bed rest wakati wa ujauzito
Sababu za kupumzika kitandani au kuanza Bed rest wakati wa ujauzito ni pamoja na;
– Mjamzito Kuwa kwenye hatari ya kupata tatizo la kifafa cha mimba(Preeclampsia/eclampsia)
– Kuvuja Damu Ukeni wakati wa ujauzito(Vaginal bleeding)
Kuvuja damu ukeni wakati wa ujauzito huweza kuashiria matatizo mbali mbali ikiwemo;
Tatizo la mimba kutoka au kutishia kutoka
Tatizo la placenta previa (kondo la nyuma/placenta kufunika sehemu au eneo lote la mlango wa kizazi
Tatizo la placental abruption (kondo la nyuma/placenta kuachia lilipojishikiza kwenye ukuta wa kizazi kabla ya wakati wake).
– Mjamzito kupata uchungu kabla ya wakati wake(Premature labor): Bed rest kwa mama mjamzito inaweza kushauriwa kwa tatizo la mama mjamzito kuanza kupata uchungu wa kujifungua kabla ya wakati wake,
Ikiwa mama mjamzito huanza kupata uchungu kabla ya wiki 37 za Ujauzito, basi moja ya vitu ambavyo atashauriwa kufanya ni pamoja na kupata mapumziko kitandani au kuanza Bed rest mara moja.
– Mjamzito kuwa na tatizo la Mlango wa kizazi kulegea(Incompetent cervix): Hapa tunazungumzia ile hali ya shingo la kizazi(Cervix) kuwa dhaifu sana, na kuanza kufunguka hata kabla ya wakati wake.
Kwa hali hii,Moja ya vitu muhimu sana kwa mama huyu mjamzito ni kuanza Bed rest mara moja.
– Tatizo la Cervical effacement: ambapo mlango wa kizazi au shingo ya kizazi kwa maana ya Cervix kuwa nyembamba sana(Thinning of your cervix).
– Kuwa na mimba ya Watoto zaidi ya mmoja(twins,triplets n.k)
Bed rest kwa mama mjamzito inaweza kushauriwa pia,ikiwa mama mjamzito kabeba mimba ya watoto zaidi ya mmoja.
– Kupata matatizo katika mimba zilizopita(Previous pregnancy complications):
Bed rest kwa mama mjamzito inaweza kushauriwa ikiwa mama mjamzito ana historia ya kupata baadhi ya matatizo kwenye mimba zilizotangulia, matatizo hayo ni pamoja na;
Ujauzito/Mimba kutoka zenyewe,
Kuzaa mtoto aliyekufa(stillbirth)
Au kujifungua mapema/kabla ya wakati(premature birth).
– Kupata tatizo la mtoto kutokukua au kudumaa akiwa bado tumboni(Intrauterine growth restriction),n.k
KUMBUKA: ni muhimu kujua ni kwanini umeambiwa uanze Bed rest ukiwa mjamzito, na pia uelezewe ni aina gani ya bed rest unatakiwa kuifuata kulingana na hali yako, ikiwa ni pamoja na kujua vitu gani unapaswa kufanya na vipi hurusiwi kabsa kufanya kulingana na Hali yako.