Dalili za Ectopic pregnancy
Je,Zipi ni dalili za Mimba kutunga nje ya kizazi au Ectopic pregnancy? Hii ndyo mada ya Leo kwenye Makala hii,
Safari ya Ujauzito huanza pale ambapo yai linafanikiwa kurutubishwa na Mbegu ya Kiume(Sperm), Na baada ya Urutubishaji kawaida lingetakiwa kujishikiza kwenye Mji wa Mimba(uterus), kitendo ambacho hujulikana kama Implantation.
Ectopic pregnancy hutokea pale ambapo Mimba hutunga nje ya kizazi au kwa lugha nyingine tunasema; yai lililorutubishwa hujishikiza na kukua nje ya mji wa mimba(Outside the main cavity of the uterus).
Mara nyingi ectopic pregnancy hutokea kwenye Mirija ya Uzazi yaani fallopian tube, Na aina hii ya ectopic pregnancy hujulikana kwa kitaalam kama tubal pregnancy.
Ingawa, ectopic pregnancy huweza kutokea kwenye maeneo mengine pia ikiwemo;
- Kwenye vifuko vya Mayai(ovary),
- Sehemu ya chini ya kizazi au Cervix n.k
Mimba iliyotunga nje ya kizazi au ectopic pregnancy haiwezi kuendelea kukua na Mtoto akaishi kwani matokeo yake ni kuongeza hatari ya kupasuka mirija ya uzazi,kizazi,mama kupoteza maisha n.k Kama usipopata Msaada wa haraka.
Dalili za Ectopic pregnancy
DALILI ZA MIMBA KUTUNGA NJE YA KIZAZI
Huenda usione dalili yoyote mwanzoni. wanawake wengi ambao wana tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi(ectopic pregnancy) wanapata dalili zote za awali za ujauzito kama vile; kukosa period au kutokuona siku zao za hedhi, matiti kujaa, kichefuchefu N.k.
Ikiwa unapima ujauzito au mimba, matokeo yatakuwa mazuri tu kama kawaida na kuonyesha kwamba wewe ni mjamzito. Tofauti tu ni kwamba matatizo huanza kutokea pale ujauzito unavyozidi kukua.
– Mara nyingi, dalili za kwanza kabsa kama una tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi ni damu nyepesi kuanza kutoka ukeni na maumivu ya kiuno au nyonga.
Ikiwa damu huvuja kutoka kwenye mirija ya uzazi(fallopian tubes), unaweza kuhisi maumivu ya bega au hamu ya kuwa na haja kubwa. Dalili maalum hutegemea mahali damu inajikusanya na mishipa ipi inaathiriwa.
Ikiwa yai lililorutubishwa linaendelea kukua kwenye mrija wa fallopian, linaweza kusababisha mrija huo wa uzazi kupasuka. Matokeo yake ni Kutokwa na damu nzito ndani ya tumbo la uzazi. Dalili kama hii huweza kuhatarisha maisha,kusababisha maumivu makali ya kichwa, kuzimia na mshtuko.
#SOMA Zaidi Mimba Kutunga nje ya Kizazi,chanzo,Dalili na Tiba Hapa
Dalili zingine ni Pamoja na;
– Kuja damu Ukeni(Vaginal bleeding)
– Kupata maumivu chini ya Tumbo
– Kupata maumivu ya nyonga au Pelvis
– Kupata maumivu ya chini ya Mgongo au Kiuno
– Kupata kizunguzungu
– Mwili kuwa Dhaifu Zaidi
– Kwa Mimba ambayo imetunga kwenye Mirija ya Uzazi au fallopian tube,ikiwa mirija hii imepasuka, utapata dalili kama vile;
- Maumivu makali ya Tumbo
- Kuvuja damu Ukeni
- Wengine kuzimia
- Shinikizo la damu kuwa chini
- Maumivu ya mabega n.k
Ikiwa una Shida hii hakikisha Unapata Msaada wa TIBA Mapema au
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.