Kuhisi dalili za mimba bila kuwa na mimba
Moja ya vitu ambavyo huwachanganya wanawake wengi, ni pale ambapo wamefanya Vipimo vya UJAUZITO vinaonyesha hawana Mimba lakini wanapata dalili zote za Ujauzito/Mimba,
Period imeacha kutoka,maziwa yanavimba,unapata kichefuchefu na kutapika n.k lakini ukifanya vipimo vyako sio Mjamzito, je shida ni nini?
Hizi hapa ni baadhi ya Sababu kwanini hali hii huweza kukutokea;
(A) NI KWELI NI MJAMZITO
Inawezekana kweli una Mimba/Mjamzito lakini ukifanya vipimo vyako vinatoa Majibu Negative na Dalili zote za Mimba unazo,kwa Sababu hizi hapa;
1. Ni kweli ni mjamzito lakini umepima mapema mno
2. Ni kweli ni mjamzito lakini kiwango cha vichocheo bado kipo chini sana kiasi kwamba vipimo vya mkojo haviwezi kugundua
Unachotakiwa kufahamu ni kwamba: Usomaji wa Kipimo cha Kupima mimba kwa njia ya mkojo yaani Urinary pregnancy test maarufu kama UPT hutegemea na uwepo wa hormone au Kichocheo cha human chorionic gonadotropin(hcg),
Kama kichocheo hiki hakijazalishwa bado au kimezalishwa ila bado ni kwa kiwango kidogo sana, inakuwa vigumu kwa kipimo cha UPT kugundua na kutoa Majibu,
Hali ambayo hupelekea Majibu kuendelea kusoma NEGATIVE wakati unapata dalili zote za Mimba.
You’re pregnant, but your hormone levels are too low for an at-home test
3. Ni kweli ni Mjamzito lakini Mwili una Maji mengi kupita kiasi(overly hydrated)
Hii huweza kusababisha hata Mkojo kuwa more diluted,
Na kadri mkojo unavyokuwa More diluted ndivo huendelea kuwa na kiwango kidogo cha hCG,
Hali hii huweza kuathiri matokeo ya Kipimo chako.
4. Ni kweli ni Mjamzito,lakini hukufanya Vipimo kwa Usahihi
5. Ni kweli ni Mjamzito,lakini umetumia vipimo vilivyokwisha Muda wake(expired pregnancy tests)
6. Ni kweli ni Mjamzio,lakini ukipima Majibu ni Negative,
Zipo baadhi ya scenarios chache ambazo huweza kuleta Majibu Negative kwenye Vipimo wakati wewe ni Mjamzito,
Mfano ni kama vile;
• Shida ya Mimba kutunga Nje ya Kizazi(Ectopic pregnancy).
Hii huweza kusababisha Kutokupata Majibu Sahihi ya Ujauzito kwa Sababu Kondo la Nyuma(placenta) haliwezi kukua kama inavyotakiwa na kuathiri hata Uzalishwaji wa kichocheo cha hCG,
Hivo basi uwepo wa Kiwango kidogo cha hcg kwenye Mkojo husababisha Kipimo kushindwa kugundua Kama Una Mimba au La!.
• Tatizo la Cryptic pregnancy japo ni mara chache sana tatizo hili kutokea
• Later-state pregnancy, Hapa nazungumzia kuchelewa kufanya kipimo chako,unafanya kipimo wakati ujauzito umeshaendelea kukua zaidi bila wewe kujua,
Mara nyingi vipimo hivi vya UPT ili vitoe majibu sahihi hutegemea na kiwango cha kichocheo cha hCG ambapo vipimo hivi vimewekewa kama Mark ya kutoa Majibu sahihi,
Kama kiwango cha hCG ni kidogo sana kipimo hakiwezi kugundua na Vile vile kama kiwango cha hCG ni kingi sana kipimo hakiwezi kugundua na kutoa majibu sahihi,
Sasa kadri Ujauzito unavyokua Mkubwa zaidi ndivo kichocheo hiki cha hCG huendelea kuzalishwa zaidi na zaidi, hivo ukichelewa sana kupima,kipimo chako pia kinaweza kisikupe majibu sahihi.
Wakati ukifanya vipimo kukiwa na kiwango kikubwa sana cha hCG, vipimo huweza kumiss completely na kutoa majibu ambayo sisahihi na hii kwa kitaalam hujulikana kama “hook effect,”.
(B) SIO MJAMZITO LAKINI UNAPATA DALILI ZOTE ZA UJAUZITO
Inawezekana kweli huna Mimba/Sio Mjamzito lakini Dalili zote za Mimba unazo,kwa Sababu hizi hapa;
1. Sio Mjamzito lakini kuna Mabadiliko makubwa ya Vichocheo mwilini,
hasa mabadiliko yanayohusisha vichocheo kama vile progesterone n.k
2. Sio mjamzito lakini upo kwenye kipi ndi cha yai kutoka yaani Ovulation,
Baadhi ya Wanawake wakiwa kwenye kipindi cha Ovulation huweza kupata dalili zote za Ujauzito kama vile; matiti kuvimba,kuuma,Kupata kichefu chefu n.k
3. Sio mjamzito lakini una dalili za Uongo yaani psychosomatic symptoms,
Hali hii ya kupata Dalili zote za Mimba lakini Sio mjamzito huweza kutokea kwa baadhi ya Wanawake ambao wamekuwa wakihitaji sana kubeba mimba,
hali hii ya kutaka Sana kubeba Mimba huweza kuwafanya baadhi ya Wanawake kuanza kupata dalili zote za mimba lakini hawana Mimba(psychosomatic symptoms).
4. Sio Mjamzito ila ni madhara ya baadhi ya DAWA,
Unaweza kupata dalili zote za Ujauzito ukadhani una mimba,kumbe ni kutokana na matumizi ya baadhi ya dawa,
Hasa jamii ya Dawa ambazo zinahusisha kuongeza vichocheo mwilini.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.