Dawa ya minyoo Albendazole,ifahamu vizuri dawa hii,
Generic name yake: Albendazole Tablets na Albendazole oral suspension
Dawa hii dose yake ipo kwenye mfumo wa vidonge yaani Tablets pamoja na mfumo wa suspension(kimiminika/syrup)
- Kidonge kimoja(tablet) kina Albendazole USP 200mg, pamoja na zingine zina USP 400mg
- Albendazole suspension ina 5mls, sawa na Albendazole USP 200mg,
Dawa hii ya Albendazole ipo kwenye therapeutic Category:PO2-Anthelmintic
Njia ya matumizi ya dawa hii au Route of administration ni kupitia mdomoni yaani Oral route.
MATUMIZI YA ALBENDAZOLE(INDICATIONS)
• Dawaa hii ya Albendazole hutumika kutibu tatizo la Minyoo,
dawa hii huweza kutibu single au Mixed Infections ya;
- Enterobius Vermicularis
- Trichuris trichiura
- Ascaris Lumbricoides
- Ancylostoma duodenale
- Necator Americanus
- Strongyloides stercoralis
- Taenia spp. Capillariasis
- Cysticercosis n.k
TAHADHARI;Warnings
Dawa za Albendazole hazitumiki kwa Mama mjamzito au Mwanamke ambaye anategemea kubeba mimba kwa kipindi hicho,
Pia tahadhari nyingine ni kuhusu blood counts na Liver function tests kabla ya matibabu, pamoja na kwa mama anayenyonyesha(breastfeeding),
Weka dawa hizi mbali na watoto-Keep the medicine out of reach of children.
MADHARA(SIDE EFFECTS) YA DAWA HIZI
- Kwa wagonjwa ambao wana heavy Intestinal infection wanaweza kupata maumivu ya tumbo na kuharisha,
- Kupata hali ya kizunguzungu kwa baadhi ya watu
- Kupata maumivu ya kichwa kwa baadhi ya watu
- Na kwa wale ambao wanajioverdose huweza kupata shida ya Bone marrow depression, Leucopenia,Pancytopenia n.k
HAYO NDYO BAADHI YA MAELEZO MACHACHE KUHUSU DAWA HII YA ALBENDAZOLE.
Dawa ya Albendazole katika kutibu Minyoo.
Posti hii inahusu zaidi dawa ya Albendazole katika kutibu Minyoo, ni Aina mojawapo ya dawa ambayo usaidia kutibu Minyoo inayosababishwa na bakteria mbalimbali.
Dawa ya Albendazole Katika kutibu Minyoo.
1. Hii ni dawa ambayo imechaguliwa kutibu Minyoo katika makundi ya madawa ya kutibu Minyoo dawa hizo ni kama vile mebendazole, levamisole ,Niclosamide Thiabendazole, praziquantel na piperazine hizi ni dawa ambazo nazo zipo kwenye kundi Moja la Albendazole ambazo utibu minyoo mbalimbali, Albendazole ufanya kazi hii kwa kuzuia kutengenezwa kwa miclotube ya wadudu au bakteria ambao ushambulia mwili wa binadamu.
Kwa kufanya hivyo wadudu hawa hawawezi tena kuendelea kufanya kazi Yao ya Maambukizi kwenye sehemu mbalimbali za mwili wa binadamu.
2.Albendazole utibu vizuri pale ambapo mgonjwa utumia dawa kabla hajala chochote kwa hiyo basi dawa hizi ni vizuri zitumiwe pale asubuhi ambapo mgonjwa anakuwa hajala kitu chocho, pia ni vizuri mgonjwa akiwa anatumia dawa hii atumie pia vyakula vyenye mafuta ,dawa hizi huwa kwenye mfomo wa vidonge na kwa watoto wenye umri juu ya miaka miwili dawa Yao inakuwa kwenye maji kwa hiyo wanapaswa kuitikisa kabla ya kuitumia kwa hiyo hii dawa huwa kwenye muuundo wa vidonge na kwa watoto juu ya umri wa miaka miwili huwa kwenye mfumo wa maji.
3. Dawa hizi za Albendazole hazitumiki kwa watoto wenye umri chini ya miaka miwili kwa sababu ambao wameitumia wanasey kuwa watoto wanapatwa sana na degedege na pia wanaweza wenye mimba hawapaswi kutumia dawa ya minyoo ya Albendazole kwa hiyo baada ya kujua madhara yanayotokea kwa watoto wenye Chini ya umri wa miaka miwili wakitumia dawa hizi tunapaswa kutoa elimu ya kutosha kwa jamii Ili kuweza kuepuka madhara makubwa ambayo yanaweza kujitokeza kwa watoto na akina Mama wenye mimba iwapo wanaotumia dawa hizi kwa hiyo inabidi waambiwe wazi dawa wanazopaswa kutumia.
4. Kwa wagonjwa wanaotumia dawa hizi wanaweza kupata matokea mbalimbali ambayo ufanya miili yao kutokuwa kawaida kama vile maumivu madogo madogo ya tumbo, kichwa kuuuma, kichefuchefu, kutapika na kuharisha kwa baadhi ya wagonjwa , kizunguzungu Homa kupanda , uchovu wa mara kwa mara. Haya yakitokea kwa mgonjwa anayetumia dawa za Albendazole hasiogope Bali yataisha Ila hali ikizidi kabisa mgonjwa anapaswa kuwaona wataalamu wa afya kwa msaada zaidi.
Wasiliana na mtaalam wako wa afya kabla haujaanza, haujasimamisha au kubadili dozi ya dawa yako yeyote ile. Via BongoClass
Fahamu matumizi sahihi ya Albendazole, dawa inayotumika kutibu minyoo
Dawa za kutibu minyoo ni dawa ambazo watu wengi mtaani wanazitumia bila hata ya kutafuta ushauri wa kitaalam. Watu wengi wakiona mtoto au mtu mzima anakula sana moja kwa moja hufikiria sababu itakuwa ni minyoo.
Mtu akiona anaumwa njaa sana siku hizi hufikiria tatizo litakuwa minyoo. Leo ningependa tufahamu matumizi sahii ya dawa hizi. Albendazole ni dawa inayotumika kutibu watu na wanyama wanaosumbuliwa na ugonjwa wa minyoo.
Albendazole ikitumika vizuri kama inavyotakiwa huua kabisa vimelea vyote (sensitive parasites). Usitumie Albendazole kama una aleji (allergy) na kiambato chochote kilichopo kwenye albendazole au benzimidazole (mfano, Rabeprazole). Wasiliana na wataalam wako wa afya kama chochote kati ya hivyo viwili hapo juu kinakuhusu.
Kabla ya Kutumia Albendazole;
Kuna hali mbalimbali za kiafya zinazoweza kuingiliana na albendazole. Wasiliana na daktari wako au mfamasia kama una hali hizi zifuatazo:
• Kama ni mjamzito, unatarajia kuwa mjamzito au unanyonyesha
• Kama una dawa nyingine yeyote ambayo unatumia, au dawa asili au dietary supplement yeyote
• Kama una aleji(allergy) na dawa, chakula au kitu kingine chochote
• Kama una matatizo ya ini, macho, mifupa au kupungukiwa dawa mara kwa mara.
Zifuatazo ni baadhi ya dawa zinazo ingiliana (interact) na albendazole :
• Cimetidine, dexamethasone au praziquantel dawa hizi huangeza madhara (side effects) za albendazole.
• Theophylline, madhara (side effects) ya dawa hii huongezeka endapo mtu atachanganya na albendazole.
Huu sio muingiliano pekee unaoweza kutokea kama mtu atatumia albendazole pamoja na dawa zingine. Upo muingiliano mwingi. Wasiliana na mtaalam wako wa afya kabla haujaanza, haujasimamisha au kubadili dozi ya dawa yako yeyote ile.
Matumizi Sahihi ya Albendazole
Tumia kama ulivyoelekezwa na daktari wako. Angalia kwenye lebo ya dawa yako kwa ajili ya maelezo zaidi.
• Tumia kwa njia ya mdomo kama unashindwa kumeza kidonge kizima, unaweza kukitafuna kwanza kasha kumeza na maji kidogo.
• Kama ukisahau kumeza dozi moja kwa muda muafaka, jitahidi kunywa kabla muda haujapita zaidi. Kama muda wa kunywa dozi nyingine umefika, endelea na dozi nyingine kama kawaida, usinywe dozi mbili kwa mara moja. Kama umesahau kunywa zaidi ya dozi moja, wasiliana na daktari au mfamasia wako.
• Albendazole inaweza sababisha kizunguzungu. Madhara haya yanaweza kungezeka kama utatumia pombe na albendazole kwa wakati mmoja.
• Albendazole inabidi zitumike kwa uangalifu mkubwa kwa watoto wa chini ya mwaka mmoja kutokana na kuwa usalama wa dawa hizi kwa kundi hili la watoto bado haujafhamika vizuri.
• Usitumie albendazole kama una ujauzito au unanyonyesha. Albendazole zinaweza kusababisha madhara makubwa kwa mtoto aliyepo tumboni. Bado hakuna majibu ya moja kwa moja kama albendazole huteza kupenya na kuingia kwenye maziwa ya mama anenyonyesha. Na ikiwa utatumia dawa hii na unaujauzito wasiliana na daktari wako kwa ushauri zaidi.
Nitoe wito kwa Watanzania kuacha kutumia dawa holela bila ya kufuata ushauri wa kitaalamu.
Credits:
FORD A. CHISANZA
Pharmacist