Maneno ya mwisho ya Edward Lowassa kabla ya Kufariki.
Kutoka Monduli Mkoani Arusha @AyoTV_ ilifanya mahojiano na Fred Lowassa ambaye ni Mtoto wa kwanza wa Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Lowassa lakini pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli ambapo pamoja na mambo mengine amezungumzia jinsi Edward Lowassa alivyokuwa kwa Watoto wake na kwa Marafiki zake.
“Alikuwa ni Baba aliyependa Watoto wake, Baba mkali hakutaka utani Shuleni, na alitaka kila Jumapili twende Kanisani, kwenye kazi ya Siasa msingi ni ubunifu, uchapakazi, ujitahidi kuwa Mtu wa maridhiano”
“Mara ya mwisho naongea na Mzee aliniambia najisikia vizuri, akasema nina maumivu hapa, akaomba tumletee supu kabla halijatokea tatizo pale Muhimbili, Baba alikuwa Mwaminifu yani akisema Wewe ni rafiki yangu hata aje nani amwambie nini yeye atasema hapana huyu namwamini ni Rafiki yangu na nitahangaika nae mpaka mwisho, Lowassa hakuwahi kumsaliti Rafiki yake hata mmoja”