Sababu za mwanaume kukosa hamu ya TENDO LA NDOA
Leo tutatazama tatizo lingine linalohusiana na ufanisi wa tendo la ndoa kwa Wanaume. Kwa kuwa neno upungufu wa nguvu za kiume limekwishazoeleka mapema kutumika na watanzania walio wengi,niseme tunatazama aina nyingine ya tatizo la upungufu wa nguvu za kiume hapa.
Tafiti zinaonesha kuwa wanaume wengi hawapendi kuishi na tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa,wakati hadi 46% ya Wanawake huonesha kuridhika kuishi na tatizo hili.
Katika mada hii tutatazama nini husababisha MWANAMUME kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Ni kawaida kupoteza hamu ya tendo la ndoa kwa vipindi tofauti tofauti.
Hamu ya tendo la ndoa hupungua pia kwa kadri umri unavyoongezeka japo siyo hivyo kwa wote,maana kuna Wanaume wengi hufikia uzeeni huku wakiwa na uwezo na hamu ya kushirikiana na wenzi wao kimapenzi.
Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa ni tatizo kubwa kwa jamii kwa sasa,takribani mwanamume 1 kati ya 5 huwa na tatizo la kukosa hamu ya tendo la ndoa.
Mara nyingi limekuwa likisababishwa na matatizo ya kisaikolojia na kimaisha pia. Fuatana nami sasa ndugu mpendwa tunapoangalia sababu hizi na inawezekana ukapata msaada kupitia mada hii ikiwa una tatizo hili.
CHANZO CHA MWANAMUME KUKOSA HAMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA NI NINI?
(A) Upungufu wa homoni ya Testesterone-
Ni homoni ya kiume ambayo huimarisha misuli,huboresha uzito wa mifupa na huchochea utengenezwaji wa mbegu za kiume (sperms). Pia homoni hii huongeza hamu ya tendo la ndoa. Kupungua kwa homoni hii inayozalishwa na korodani,husababisha kupungua kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa na uzalishaji wa mbegu za kiume huwa kwa kiwango kidogo.
(B)Matumizi ya Dawa
Kutumia baadhi ya dawa huweza kupunguza uwezo wako wa kushiriki na Mke wako. Matumizi ya dawa kama za high blood pressure kama vile ACE na BLOCKER huweza kusababisha uwezo wa kufanya mapenzi kupungua na hamu ya tendo la ndoa kupotea kabisa.
(C)Mfadhaiko
Mfadhaiko huathiri utendaji kazi wa mwili wako wote. Mfadhaiko humfanya mtu apoteze kuvutiwa na kazi alizozoea kuzifanya hapo kabla ikiwa ni pamoja na tendo la ndoa. Imethibitika kuwa dawa za kupunguza mfadhaiko pia hupunguza hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mtumiaji.
(D)Magonjwa ya muda mrefu
Kama unajisikia vibaya kutokana na ugonjwa wa muda mrefu,kufanya tendo la ndoa haitakuwa hitaji lako la kwanza. Magonjwa kama kansa hupunguza kiwango cha mbegu zako na hivyo hamu ya tendo la ndoa kupungua.
(E) Kukosa usingizi
Imebainika kuwa tatizo la kukosa usingizi husababisha kupungua kwa kiwango cha homoni ya testesterone. Kupungua kwa homoni ya testesterone husababisha kupungua kwa hamu ya kufanya mapenzi pia.
(F) Msongo wa mawazo
kwa mtu mwenye msongo uwezo wake wa kufanya tendo la ndoa hupungua. Hii ni kwa sababu msongo husababisha hitilafu kwenye mfumo wa homoni. Na hii huweza kupelekea mishipa ya ATERI kubana na kuzuia damu kufikia sehemu muhimu zinazohusika na ufanyaji wa tendo la ndoa.
(G) Kutojiamini
Haitawezekana kufanya tendo la ndoa kama wewe mwenyewe huamini. Kutojiamini hupelekea wasiwasi ambayo husababisha mvurugiko wa homoni zinazohusika kuongeza hamu na ufanyaji wa tendo la ndoa.
(H)Pombe na Madawa ya kulevya
Matumizi ya pombe husababisha kupungua kwa uwezo wa kufanya tendo la ndoa. Matumizi ya madawa ya kulevya kama marijuana huharibu utendaji kazi wa tezi ya PITUITARIES inayoratibu utengenezwaji wa homoni ya TESTOSTERONE.
(I) Uume kushindwa kudinda
Kukosa hamu ya tendo la ndoa ni matokeo ya Uume kushindwa kusimama. Kama ulipatwa na tatizo la Uume kushindwa kusimama husababisha wasiwasi na kutojiamini. Hii ni kwa sababu ya kufikiri kwamba huenda ikatokea tena. Hata hivyo uume kushindwa kusimama ni dalili ya uwepo wa tatizo kubwa la kiafya kama vile magonjwa ya moyo.
(J) Unene uliopitiliza-Na kitambii
Unene husababisha kupungua kwa homoni ya testesterone na kusababisha hamu ya tendo la ndoa kupungua. Pia unene huweza kusababisha magonjwa ya moyo na high blood pressure,ambayo kwa pamoja husababisha kupungua kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa.
(K) Mahusiano baina ya Wanandoa
Kama kuna magomvi,matukano na kupigana kati ya Wanandoa hamu ya kushiriki pamoja pia hupungua kama sio kutoweka kabisa. Lakini pia kama Wanandoa hawa wako mbali mbali pia hupelekea hamu ya kufanya mapenzi kupungua.
(L) Umri mkubwa
Utengenezwaji wa homoni ya testesterone inayohusika na kuongeza hamu ya tendo la ndoa hupungua kwa kadri umri unavyoongezeka. Wanaume mara nyingi huanza kuhisi tatizo hili kuanzia miaka 60 hadi 65. Kupungua kwa homoni hii husababisha kupoteza hisia za tendo la ndoa na kuchelewa kufika kileleni
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.