Kesi za kipindupindu nchini Zambia zazidi 3,000
Idadi ya kesi za kipindupindu nchini Zambia imeongezeka na kufikia 3,189 tangu mlipuko wa ugonjwa huo ulipotokea mwezi Januari mwaka jana 2023.
Mamlaka za afya nchini humo zimesema, ugonjwa huo uligunduliwa katika wilaya nne za mkoa wa Lusaka, na kuenea katika wilaya nyingine zilizo katikati ya nchi hiyo.
Jumatatu wiki hii, rais wa Zambia, Hakainde Hichilema alisema anajitahidi kuiwezesha Zambia kuwa kituo cha uzalishaji wa chanjo ya kipindupindu.