Mwimbaji wa nyimbo za Injili wa Brazil Pedro Henrique aanguka na kufa wakati wa performance.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea na kuleta majonzi makubwa kwa mashabiki wa mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Brazili Pedro Henrique alipoanguka jukwaani katikati ya onyesho/performance na kufariki.
Pedro alikuwa akitumbuiza kwenye hafla ya Kikristo Jumatano usiku, wakati alianguka sakafuni ghafla na kupoteza fahamu.
Kanda za video zinaonyesha Pedro kwenye ukingo wa jukwaa akitangamana na umati na kuimba wimbo “Vai Ser Tão Lindo” kisha alionekana kupoteza Fahamu, akianguka chali mbele ya bendi yake na kuanguka chini.
Baada ya kuzimia, watu walimkimbilia kumsaidia huku umati uliokuwa na hofu ukitazama tukio hilo kwa mshtuko.
Pedro mwenye umri wa miaka 30 alikimbizwa kutoka kwenye ukumbi wa tamasha hadi kliniki ya karibu ya matibabu, ambapo alitangazwa kuwa amefariki,
Na lebo yake ya muziki, Todah Music, inasema alipata mshtuko mkubwa wa moyo.