Faida za Mafuta ya Mawese(Palm Oil),Soma hapa
Leo nmekuchambulia baadhi ya faida za Mafuta ya Mawese yaani Palm Oil, na Hizi ni baadhi ya Faida hizo;
1. Kusaidia kuboresha uwezo wa macho kuona,
Hii ni kutokana na uwepo wa kiwango kikubwa cha Beta Carotene ndani ya mafuta ya Mawese, ambacho hubadilishwa na kuwa vitamin A,
Vitamin A ni msaada mkubwa katika kuboresha afya ya macho.
2.Kusaidia Kulainisha Ngozi yako,
Hii ni kutokana na uwepo wa agents maarufu kama Re-fattening agents ambazo husaidia kurudisha mafuta asilia ya ngozi pamoja na unyevu unyevu kwenye ngozi.
3. Kusaidia Kupunguza hatari ya Saratani za aina mbali mbali,
Kuwa na kiwango kikubwa cha Antioxidants
4. Kuboresha afya na ukuaji wa nywele
5. Pia Mafuta ya Mawese hayana Trans-Fat zozote yaani ni Zero Trans-Fat,
ila Yana Unsaturated fats
6. Husaidia kuzuia hatari ya mtu kupata magonjwa mbali mbali ya Moyo
7. Mafuta ta Mawese yana kiwango kikubwa cha Vitamins mbali mbali, kama vile; Vitamin K, Vitamin D, Vitamin A, na Vitamin E
8. Mafuta ya Mawese ni msaada pia kwa mama Mjamzito,
Kutokana na wingi wa Virutubisho kama vile Vitamin D,A na E,
ambavyo ni muhimu sana kwenye afya na Ukuaji wa Mtoto tumboni.
9. Kusaidia kuupa Mwili nguvu(Energy)
10. Na Kusaidia katika urekebishaji wa vichocheo mbali mbali mwilini.
NB: Ingawa ni mara chache sana huweza kuleta madhara ila matumizi ya kiwango kikubwa zaidi kuliko kawaida cha Mafuta ya Mawese huweza kuleta madhara mbali mbali kama vile;
Kubadilisha rangi ya ngozi na kuwa ya yanjano(yellowish) na hii ni kutokana na uwepo wa kiwango kikubwa cha Carotenes.