Matumizi ya tumbaku yapungua licha ya juhudi za sekta ya tumbaku kuhatarisha maendeleo
Ulimwenguni kote kuna watumiaji wa tumbaku bilioni 1.25 kwa mujibu wa makadirio yaliyotolewa leo ya utafiti wa hivi karibuni wa Shirika la Afya Duniani, WHO, mwelekeo wa tumbaku.
Mienendo katika mwaka wa 2022 inaonesha kuendelea kupungua kwa viwango vya matumizi ya tumbaku duniani kote. Takribani mtu mmoja kati ya watu wazima watano duniani kote hutumia tumbaku ikilinganishwa na mtu 1 kati ya watu 3 mwaka wa 2000.
Ripoti hiyo inaonesha kuwa nchi 150 zinafanikiwa kupunguza matumizi ya tumbaku. Brazili na Uholanzi zinaona mafanikio baada ya kutekeleza njia za udhibiti wa tumbaku za MPower, huku, Sikiliza kuhusu Mpower.
Brazili ikipunguza kiasi cha 35% tangu 2010 na Uholanzi katika hatihati ya kufikia lengo la 30%.
Kulingana na Dkt. Ruediger Krech, Mkurugenzi wa Idara ya WHO ya Kukuza Afya, “mafanikio mazuri yamepatikana katika udhibiti wa tumbaku katika miaka ya hivi karibuni, lakini hakuna wakati wa kuridhika. Ninashangazwa na jinsi tasnia ya tumbaku itakavyotafuta faida kwa hasara ya maisha mengi. Tunaona kwamba dakika ambayo serikali inafikiria kuwa imeshinda vita dhidi ya tumbaku, tasnia ya tumbaku inachukua fursa hiyo kudanganya sera za afya na kuuza bidhaa zao hatari.”
Shirika la Afya Ulimwenguni linaongeza ufahamu juu ya madhara ya matumizi ya tumbaku na uvutaji wa moshi wa sigara.
WHO inazitaka nchi kuendelea kuweka sera za kudhibiti tumbaku na kuendelea kupambana na tasnia ya tumbaku kuingilia.
Hivi sasa, WHO Kanda ya Kusini-Mashariki mwa Asia ina asilimia kubwa zaidi ya watu wanaotumia tumbaku kwa 26.5% huku Kanda ya Ulaya ikiwa haiko mbali kwa 25.3%. Ripoti hiyo inaonesha kuwa ifikapo mwaka wa 2030, WHO Kanda ya Ulaya inakadiriwa kuwa na viwango vya juu zaidi duniani vya matumizi ikiwa na zaidi ya 23%. Viwango vya matumizi ya tumbaku miongoni mwa wanawake katika kanda ya Ulaya ya WHO ni zaidi ya mara mbili ya wastani wa kimataifa na vinapungua polepole zaidi kuliko katika maeneo mengine yote.
Ingawa idadi imepungua kwa miaka mingi, dunia itapunguza matumizi ya tumbaku kwa 25% ifikapo 2025, na kukosa kufikia lengo la kimataifa hiari la kupunguza 30% kutoka kwa msingi wa mwaka wa 2010. Ni nchi 56 tu duniani zitafikia lengo hili, chini ya nchi nne tangu ripoti ya mwisho mwaka wa 2021.
Kiwango cha matumizi ya tumbaku kimebadilika kidogo tangu mwaka wa 2010 katika baadhi ya nchi, wakati nchi sita bado zinashuhudia matumizi ya tumbaku yakiongezeka: Congo, Misri, Indonesia, Jordan, Oman, na Jamhuri ya Moldova.
WHO inazitaka nchi kuharakisha juhudi za kudhibiti tumbaku kwani bado kuna kazi kubwa ya kufanywa. “Kielezo cha kuingilia kwa sekta ya Tumbaku Duniani 2023”, iliyochapishwa na STOP na Kituo cha Kimataifa cha Utawala Bora katika Udhibiti wa Tumbaku, inaonesha kuwa juhudi za kulinda sera ya afya kutokana na kuingiliwa kwa sekta ya tumbaku imezorota kote ulimwenguni.
WHO inasema takriban nusu ya watoto wote duniani wanaripotiwa kupumua hewa iliyochafuliwa na moshi wa tumbaku,. (Maktaba)
Uchunguzi wa nchi mara kwa mara unaonesha kuwa watoto wenye umri wa miaka 13-15 katika nchi nyingi wanatumia tumbaku na bidhaa za nikotini. Ili kulinda vizazi vijavyo na kuhakikisha kuwa matumizi ya tumbaku yanaendelea kupungua, WHO itafanya mahususi Siku ya Kutotumia Tumbaku mwaka huu kwa Kuwalinda watoto dhidi ya kuingiliwa na tasnia ya tumbaku.
Mwezi ujao nchi zinatazamiwa kukutana nchini Panama kwa ajili ya Kikao cha 10 cha Mkutano wa Mkakati wa WHO wa Kudhibiti Tumbaku (FCTC) ambapo sekta ya tumbaku itajaribu kushawishi sera za afya za kimataifa kwa kutoa motisha za kifedha na zisizo za kifedha. kuingilia kati haki za nchi. kulinda afya za watu wao. Kuimarisha FCTC ya WHO ni kipaumbele cha afya duniani kilichoainishwa katika Malengo ya Maendeleo Endelevu. WHO iko tayari kuunga mkono nchi katika kutetea hatua zilizothibitishwa za udhibiti wa tumbaku licha ya kuingiliwa kwa tasnia.