TATIZO LA MISULI YA UKE KUBANA AU KUKAZA(VAGINISMUS),CHANZO,DALILI NA TIBA YAKE
Vaginismus,hili ni tatizo la misuli ya uke kubana au kukaza yenyewe pasipo kupanga au bila hiari ya mwanamke mwenyewe,na tatizo hili la misuli ya uke kubana hutokea pale ambapo kuna kitu chochote kinatakiwa kupitishwa ukeni kama vile uume wakati wa tendo la ndoa n.k,
Hali hii husababisha mwanamke kutokufurahia kabsa tendo la ndoa,uume kushindwa kupita au kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa au wakati akiguswa maeneo yaliyo karibu na uke,
Kumbuka; Kuna watu wengi huchanganya maumivu wakati wa tendo la ndoa yaani Dyspareunia pamoja na tatizo hili la misuli ya uke kubana yaani vaginismus, fahamu kwamba vitu hivi ni tofauti,japo mtu mwenye tatizo la misuli ya uke kubana huweza kupata tatizo la maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
CHANZO CHA TATIZO HILI LA MISULI YA UKE KUBANA
Mpaka sasa hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo husababisha tatizo hili,ila tafiti zinaonyesha kuna baadhi ya sababu mbali mbali ambazo huongeza uwezekano wa mtu kupatwa na tatizo hili la misuli ya uke kubana,na sababu hizo ni kama vile;
- Mwanamke kuwa na historia ya kufanyiwa vitendo vya kikatili hapo nyuma kama vile kubakwa au kuingiliwa kinyume na maumbile bila ridhaa yake
- Mwanamke kuwa na historia ya kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
- Mwanamke kupata majeraha sehemu za siri
- Tatizo la hofu na wasiwasi mkubwa wa kufanya tendo la ndoa n.k
DALILI ZA TATIZO HILI LA MISULI YA UKE KUBANA NI PAMOJA NA;
• Misuli ya uke kukakamaa na kubana yenyewe pale unapojaribu kuingiza kitu chochote ukeni
• Maumivu makali sana wakati wa tendo la ndoa,kumbuka sio kila maumivu makali wakati wa tendo la ndoa basi chanzo chake ni tatizo la misuli ya uke kubana
• Mwanamke kuingiwa na hofu ya kuingiza kitu chochote ukeni
• Mwanamke kukosa kabsa hamu ya tendo la ndoa hasa pale anapofikiria uume utakavyopita ukeni
• Mwanamke kuhisi hali ya kuungua ukeni au kuchoma wakati kitu chochote kikiwekwa ukeni au kuguswa maeneo ya kuzunguka uke
MATIBABU YA TATIZO LA MISULI YA UKE KUBANA
Zipo njia mbali mbali za kumsaidia mwanamke mwenye tatizo hili la misuli ya uke kubana na njia hizo ni kama vile;
✓ Mwanamke kufundishwa jinsi ya kufanya mazoezi ya kubana misuli ya uke au mazoezi ya kudhibiti utendaji kazi wa misuli ya ukeni ambapo yote kwa kitaalam hujulikana kama Kegel exercise
✓ Mazoezi hayo pia huhisisha zoezi ya kupitisha kitu ukeni ili kusaidia misuli ya ukeni kufanya kazi vizuri,kumbuka unatakiwa kufanya mazoezi haya kwa maelekezo kamili kutoka kwa wataalam wa afya
✓ Pia kuna matumizi ya dawa mbali mbali za kusaidia utendaji kazi wa misuli ya ukeni na kuondoa hali ya misuli ya ukeni kukakamaa pamoja na kubana.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.