JINSI YA KUJIKINGA NA PID
PID-Pelvic Inflammatory disease,huu ni ugonjwa ambao unahusu maambukizi ya Bacteria kwenye via vya uzazi vya mwanamke.
soma zaidi hapa kuhusu dalili zake:
Njia za kukusaidia kujikinga na Ugonjwa wa PID ni pamoja na;
- Kufanya safe sex au kuepuka ngono zembe
- Epuka tabia ya kuwa na wapenzi wengi yaani multiple sexual partners
- Ongea na wataalam wa afya kuhusu njia salama za uzazi wa mpango,
kwani baadhi ya njia hizo hazikulindi na Pid Bali huongeza hatari ya kupatwa na PID,
tumia njia kama Condom ni salama zaidi kukukinga na magonjwa mengi ya zinaa ikiwa ni pamoja na mimba
- Fanya vipimo vya magonjwa ya Zinaa mara kwa mara,
Kumbuka; Kama upo kwenye hatari ya kupata magonjwa ya zinaa basi utakuwa kwenye hatari zaidi ya kupata PID pia.
Hivo ukijilinda na magonjwa ya zinaa au kupata tiba kamili unakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuepuka PID vile vile.
- Hakikisha na mwenza wako au mpenzi wako na yeye anafanya vipimo kabla ya kuanza kushiriki tendo la ndoa,
na epuka kufanya naye mapenzi kama ana dalili zozote za magonjwa ya zinaa mpaka apate tiba
- Pia unashauriwa kuepuka kuweka vitu kama vidole,Douches,au sabuni zenye kemikali kali ukeni. N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.