Dalili za Saratani ya Mlango wa Kizazi: Jinsi ya Kujikinga na Saratani ya Mlango wa Kizazi
Saratani ya mlango wa kizazi ni moja ya aina ya saratani hatari ambayo inaweza kuathiri wanawake wengi. Saratani hii inaanza katika seli za mlango wa kizazi, ambayo ni sehemu ya chini ya uzazi wa mwanamke.
Saratani ya mlango wa kizazi inaweza kuwa na athari kubwa kwa maisha ya mwanamke, lakini inaweza kugunduliwa na kutibiwa ikiwa itagunduliwa mapema.
Katika makala haya, tutazungumzia juu ya dalili za saratani ya mlango wa kizazi, sababu, hatari na jinsi ya kujikinga na saratani ya mlango wa kizazi.
Kwa mujibu wa Vituo vya Kudhibiti na kuzuia magonjwa yaani Centers for disaeses control and Prevention-CDC
" Kila Mtu mwenye Mlango wa kizazi(cervix) yupo kwenye hatari ya kupata Saratani ya mlango wa kizazi,
Na kwa asilimia kubwa hutokea kwa wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka 30, huku sababu kubwa ya tatizo hili la saratani ya Mlango wa kizazi ni maambukizi ya virusi vya human papillomavirus (HPV) "
Dalili za Saratani ya Mlango wa Kizazi
Dalili za saratani ya mlango wa kizazi zinaweza kutofautiana kulingana na hatua ya saratani. Hapa kuna dalili za saratani ya mlango wa kizazi:
1. Mwanamke kuvuja damu katikati ya mzunguko wa hedhi au baada ya kumalizika kwa hedhi,
2. Kuvuja damu baada ya tendo la ndoa
3. Maumivu wakati wa tendo la ndoa
4. Maumivu wakati wa kukojoa
5. Kutokwa na uchafu usio wa kawaida ukeni
6. Kuongezeka kwa kiasi cha uchafu ukeni
7. Mabadiliko katika hedhi yako ya kawaida (kupata hedhi ambayo ni nyingi au ndefu kuliko kawaida)
8. Maumivu ya tumbo na mgongo
9. Kupungua uzito kwa kasi bila sababu yoyote
10. Kukosa hamu ya tendo la ndoa n.k
Sababu za Saratani ya Mlango wa Kizazi
Saratani ya mlango wa kizazi inasababishwa na maambukizi ya Virusi vya Human papillomavirus (HPV),
ambapo ni miongoni mwa virusi ambavyo unaweza kupata wakati wa kujamiiana.
HPV inaweza kuambukizwa kupitia ngono au kwa kugusana kwa ukaribu sana na ngozi iliyoharibiwa.
Maambukizi ya HPV hayana dalili, kwa hivyo inaweza kuwa ngumu kujua ikiwa umeambukizwa au la.
Hatari ya Saratani ya Mlango wa Kizazi
Kuna sababu kadhaa ambazo zinaweza kuongeza hatari ya mwanamke kupata saratani ya mlango wa kizazi. Sababu Hizi ni pamoja na:
- Kuwa na historia ya maambukizi ya HPV
- Kuanza ngono katika umri mdogo
- Kuwa na wapenzi wengi
- kufanya ngono zembe au mapenzi bila kinga kama vile condom n.k
Jinsi ya Kujikinga na Saratani ya Mlango wa Kizazi
Kuna hatua kadhaa ambazo unaweza kuchukua ili kujikinga na saratani ya mlango wa kizazi. Hapa kuna njia kadhaa za kujikinga na saratani ya mlango wa kizazi:
1.Chanjo ya HPV: Chanjo ya HPV inapatikana kwa wasichana na wavulana wenye umri wa miaka 9 hadi 45.
Chanjo hii inaweza kusaidia kuzuia maambukizi ya HPV ambayo husababisha saratani ya mlango wa kizazi.
2. Kufanya vipimo vya mara kwa mara:
Ni muhimu kufanya vipimo vya mara kwa mara ili kugundua saratani ya mlango wa kizazi mapema.
Vipimo hivi ni pamoja na vipimo vya Pap smear na vipimo vya HPV.
3. Kuepuka ngono zisizo salama: Unapaswa kujiepusha na ngono zisizo salama ili kuzuia maambukizi ya HPV na saratani ya mlango wa kizazi.
FAQs: Maswali Yanayoulizwa Sana Kuhusu Saratani ya Mlango wa Kizazi
Hitimisho
Saratani ya mlango wa kizazi ni moja ya aina hatari za saratani ambazo zinaweza kuathiri wanawake wengi. Walakini, saratani hii inaweza kugunduliwa na kutibiwa ikiwa itagunduliwa mapema.
Kwa hivyo, ni muhimu kufanya vipimo vya mara kwa mara na kuchukua hatua za kujikinga ili kuzuia saratani ya mlango wa kizazi.
Kwa kufanya hivyo, utaweza kuishi maisha yenye afya na furaha bila ya kuhangaika na saratani ya mlango wa kizazi.
Dalili za Saratani ya Shingo ya Kizazi,Soma zaidi hapa...!!!!!
DALILI NA VIASHIRIA VYA KUWA NA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI.
SARATANI NI NINI?
Saratani ni hali ya ukuaji wa seli hai za mwili usio wakawaida au ulizidi kiwango,Kwahyo basi, Saratani ya shingo ya kizazi ni ukuaji usio wa kawaida wa seli hai zilizopo au zinazounda eneo la shingo ya kizazi.
Chanzo cha Saratani ya Shingo ya Kizazi
Saratani ya Kizazi au saratani ya shingo ya kizazi husababishwa na Kirusi aitwaye HUMAN PAPILLOMA VIRUS (HPV).
kirusi huyu ndyo Mhusika mkuu wa Tatizo hili ambapo kitaalam tatizo hili la Saratani ya shingo ya Kizazi hujulikana kama "cervical Cancer"
KUNDI LILILOPO KATIKA HATARI YA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI
➖ Watu wanaoanza kushiri tendo la Ndoa au mapenzi wakiwa na umri mdogo mfano kabla ya miaka 18 au 20.
➖ Watu wenye wapenzi wengi yaani Multiple parteners
➖ Wanawake wenye Umri mkubwa mfano miaka 50 na kwenda mbele
➖ Kuzaa katika umri mkubwa mfano miaka 48.
➖ wanaotumia dawa zozote zinazohusu kuongeza uzalishaji wa seli hai za Mwili.
?DALILI ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI
Saratani ya shingo ya kizazi katika hatua za awali haina dalili au viashiria vyovyote.
- Kutokwa na damu katika tupu ya mwanamke (vagina) ambayo sio ya kawaida. Damu hii inaweza kuwa matone, au damu inayotoka katikati ya mzunguko wa hedhi (yaani baada ya hedhi kabla ya hedhi inayofuata) au damu itokayo kwa mwanamke ambae ameacha kupata hedhi.
- Kutokwa na damu baada ya kujamiana baada ya tendo la ndoa.
- Maumivu wakati wa kujamiana.
Dalili za saratani iliyosambaa ni kama zifuatavyo
- Kutokwa na majimaji ukeni kusiko kawaida yenye harufu na maumivu ya tumbo chini ya kitovu.
- Kupungua kwa hamu ya kula
- Kupungua uzito
- Kuhisi uchovu
- Maumivu ya nyonga
- Maumivu kwenye mgongo
- Maumivu ya mguu
- Mguu mmoja kuvimba
- Kutokwa na damu nyingi kwenye tupu ya mwanamke
- Kuvunjika mifupa (bone fractures)
- Kutokwa na mkojo au kinyesi kwenye tupu ya mbele ya mwanamke.
MADHARA YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI
(1) Kupoteza maisha kwa Mwanamke
(2) Kutolewa kizazi chote na kupoteza uwezo wa mwanamke kuzaa tena
(3) Kuvuja damu na kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
(4) Kutokwa na harufu kama ya kitu kilichooza Ukeni
MATIBABU YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI
Endapo tatizo hili litakugundulika katika stage za mwanzoni kabsa,mwanamke atapata tiba na atapona kabsa.Lakini kama akachelewa na saratani hiii au kansa hii ikafika stage iv ni ngumu kupona.
Kwahyo basi kuna umuhimu sna wa Kujichunguka kila wakati na pale unapoona mabadiliko yoyote mwilin,wahi hosptal kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.