Tatizo la kujing'ata Ulimi ukiwa usingizini na dawa yake
Tatizo hili huweza kutokea kwa mtu yoyote, watoto mpaka watu wazima,
Mara nyingi unaweza Kujing'ata Ulimi ukiwa unakula, ila kwenye tatizo hili la kujing'ata Ulimi hutokea wakati umelala.
Na watu wenye tatizo hili la kujing'ata Ulimi Wakiwa wamelala,wanakuwa kwenye hatari ya Kupata vidonda kwenye Ulimi, na Kupata maambukizi ya magonjwa kwa Urahisi zaidi.
CHANZO CHA TATIZO HILI LA KUNG'ATA ULIMI UKIWA UMELALA
Tatizo la Seizures pamoja na hali nyingine yoyote ambayo husababisha misuli ya uso kukakamaa(facial muscle spasms) huweza kusababisha mtu kung'ata Ulimi akiwa amelala,
Sababu zingine ni pamoja na;
- Tatizo la kusaga meno au Bruxism, Hili ni tatizo ambalo huhusisha kusaga meno na kubana meno na huweza kutokea pia ukiwa umelala,
Tatizo hili huathiri meno pamoja na Taya, Pia huweza kuchangia Mtu kung'ata Ulimi pamoja na Mdomo wakati amelala.
- Tatizo la Misuli ya Uso kukakamaa(Facial muscle spasms), Hii hutokea sana kwa watoto wadogo na huweza kupelekea mpaka kidevu kutetemeka mtoto akiwa amelaa,
watu ambao wanapata shida hii hawawezi kudhibiti(control) misuli ya Uso pamoja na Taya wakiwa wamelala,na mara kwa mara wanang'ata Ulimi wakiwa Usingizini, hali hii kwa kitaalam pia hujulikana kama "faciomandibular myoclonus.”
- Matumizi ya Dawa Haramu au dawa za kulevyia, dawa hivi huweza kupelekea mtu kupata tatizo la bruxism,
Kisha kupelekea kujing'ata Ulimi,kuumia mdomoni,kwenye meno n.k
Pia baadhi ya tafiti zinaonyesha dawa hizi huweza kuongeza hamu ya mtumiaji kujing'ata Ulimi au Mdomo, na kupunguza uwezo wa Taya Kufunguka.
- Ugonjwa wa Lyme(Lyme disease), Ugonjwa huu huweza kuathiri mfumo wa fahamu yaani central nervous system pamoja na bodily reflexes,
Hii huweza kupelekea kujing'ata Ulimi au mashavu kwa ndani. Dalili zingine za ugonjwa huu ni pamoja na;
• Kuhisi baridi sana au joto sana
• Mwili kuchoka kupita kiasi
• Kuanza kupata shida wakati wa kuongea (slurred speech)
• Mtu kuharisha mara kwa mara
• Kupata shida ya kuona vizuri
• Kupata maumivu mwili mzima,mwili kutetemeka n.k
- Kupata tatizo la mwili kutetemeka wakati wa usiku(Nighttime seizures), hii huchangia sana tatizo la kung'ata Ulimi ukiwa umelala,
Watu wenye ugonjwa wa Kifafa hushindwa kabsa kudhibiti Mwili wakati hali hii ya kutetemeka(Seizures) inatokea, Hii huweza kupelekea Kujing'ata Ulimi.
- Tatizo la Rhythmic movement disorder, hali hii hutokea zaidi kwa watoto, ambapo mtoto akiwa amelala au Kusinzia huweza kutoa sauti za kuvuma, miondoko ya mwili kama vile kujitikisa na kugonga kichwa, au kujiviringisha. Misogeo hii inaweza kuwa ya haraka na inaweza kusababisha kuuma kwa ulimi.
- Kukosa usingizi hakusababishi Mtu kung'ata ulimi, lakini kung'ata Ulimi ni jambo la kawaida kwa watu wengi wenye tatizo la kukosa usingizi.
Hii ni kwa sababu watu wenye tatizo la kukosa usingizi huweza kuwa na shida ya misuli mdomoni kulegea isivyo kawaida wakati wa kulala n.k
BAADHI YA DALILI ZA MTU MWENYE TATIZO LA KUNG'ATA ULIMI WAKATI AMELALA
✓ Ulimi kuvuja damu
✓ Ulimi kubadilika rangi na kuwa mwekundu zaidi
✓ Ulimi Kuvimba
✓ Kupata maumivu kwenye Ulimi
✓ Ulimi kuwa na alama za kung'atwa
✓ Ulimi kuwa na Vidonda n.k
MATIBABU YA TATIZO HILI LA KUNG'ATA ULIMI WAKATI UMELALA
- Tiba ya tatizo hili huhusisha chanzo chake kwa asilimia mia, mfano kama tatizo ni bruxism basi lazima tatizo hili lidhibitiwe n.k
Hivo basi ni lazima uongee na wataalam wa afya na kufanyiwa vipimo zaidi ili kujua chanzo cha tatizo lako