Maumivu ya chini ya kitovu kwa mjamzito
Nini Husababisha Maumivu ya Chini ya Kitovu au tumbo Wakati wa Ujauzito?
Hili ni Swali ambayo wanawake wengi wajawazito hujiuliza,baada ya kuona shida hii, Leo tumekuchambulia kila kitu ili uweze kujua.
Wakati wa ujauzito,hali ya maumivu chini ya kitovu au tumbo inaweza kutokea kwa sababu ya maumivu ya misuli, gesi, kuvimbiwa,kukosa choo au kupata choo kigumu tatizo ambalo hujulikana kama Constipation, au sababu mbaya zaidi ya Kiafya kama vile maambukizi au leba kutokea kabla ya wakati(hapa tunazungumzia preterm labor).
Kuanzia siku ya kwanza ya kupata dalili za mimba(ulipotambua kuwa ulikuwa mjamzito) hadi kuanza kupata maumivu ya kiuno unayohisi sasa,kadri ukuaji wa mtoto wako unapoongezeka, kila siku ya ujauzito unaweza kuona mabadiliko mbali mbali mwilini mwako ambayo huja na aina fulani ya usumbufu,
Pengine Inaweza kuwa ni Ujauzito wako wa kwanza kwahiyo huna Uzoefu wa aina yoyote, Maumivu ya chini ya kitovu kwa mjamzito ni miongoni mwa hali ambazo huwasumbua wanawake wengi pindi wakiwa wajawazito.
Swali moja ambalo unaweza kuhangaika nalo linahusu; Ni wakati gani wa kumjulisha Mtoa huduma wako wa afya ikiwa unahisi maumivu chini ya kitovu na wewe ni mjamzito?. Kwani hutaki chochote kiende vibaya kwako na kwa mtoto wako anayekua.
Ili kukusaidia kujua sababu hasa za maumivu hayo ya chini ya kitovu au tumbo, tumejumuisha orodha ya sababu zinazoweza kusababisha maumivu hayo pamoja na baadhi ya ishara za onyo zinazomaanisha kuwa ni wakati wa kumjulisha mtoa huduma wako wa Afya Mapema.
Chanzo cha Maumivu ya chini ya kitovu kwa mjamzito
Ni sababu gani zinazopelekea maumivu ya chini ya kitovu au tumbo wakati wa ujauzito?
Baadhi ya sababu kubwa za maumivu ya chini ya kitovu au tumbo wakati wa ujauzito ni pamoja na:
1. Maumivu kutokana na ligaments;
Ligament ni mkusanyiko wa tishu( a band of connective tissue) ambazo huunganisha mifupa, joints or Au viungo mbali mbali vya mwili.
Ligaments kwenye fupanyonga(pelvis) zinazoshikilia uterasi yako hunyooshwa Zaidi wakati tumbo lako likikua na kupanuka, Na Kwa sababu mimba huweka mkazo zaidi kwenye mishipa hii, ligaments zinaweza kuwa na mkazo na kutanuka kupita kiasi, Hali hii huweza kupelekea wewe kupata maumivu ya chini ya kitovu.
Hii hutokea Zaidi kwenye kipindi cha second na third trimesters kwenye Ujauzito wako,ambapo unahisi maumivu na usumbufu hasa ukitembea haraka.
Trimesters; Tunazungumzia kipindi cha miezi mitatu mitatu(3) ya Ujazito, mfano tukisema first trimester tunamaanisha miezi 3 ya mwanzo ya Ujauzito n.k.(kumbuka vizuri maana ya neno hili Trimester maana tutalitumia sana kwenye mada hii).
Unachotakiwa kufahamu pia; Aina ya maumivu haya ambayo chanzo chake ni Ligaments sio Maumivu ya kudumu, hutokea kwa muda mfupi kisha kupotea.
2. Tatizo la Gas;
Tatizo la Gas kujaa tumboni huweza kutokea wakati wowote wa Ujauzito, na hali hii huchangiwa zaidi na;
- Kutanuliwa kwa misuli ya utumbo kwa sababu ya kiwango kikubwa cha hormones aina ya progesterone kipindi cha Ujauzito.
- Pia kuongezeka zaidi kwa ukubwa wa Uterus wakati mtoto anakua,hali ambayo huweka mgandamizo zaidi kwenye viungo vyako na kupunguza umeng'enyaji wa chakula(slowing digestion).
Hali hii ya kujaa gesi tumboni huweza kupelekea tatizo la maumivu ya chini ya kitovu ukiwa mjamzito, Ikiwa unapata maumivu kutokana na kuwa na gesi tumboni, unaweza kula kidogo kidogo ila mara kwa mara. Unaweza pia kujaribu mazoezi yatakayokusaidia usagaji wa haraka wa chakula, lakini pia tambua na kisha uepuke vyakula vinavyosababisha gesi zaidi kwako.
3. Tatizo la kukosa choo au kupata choo kigumu(Constipation);
Takriban robo ya wanawake wajawazito wanapatwa na tatizo hili la kukosa choo na kupata choo kigumu wakati fulani wa ujauzito. Lishe isiyo na nyuzinyuzi(fibers),kutokunywa vimiminika vya kutosha kama maji, matumizi ya virutubishi vya madini ya chuma, na kubadilika-badilika kwa homoni ni baadhi tu ya sababu zinazoweza kuchangia tatizo hili kujitokeza.
Hali hii Pia huongeza hatari ya mama mjamzito kupata maumivu ya chini ya kitovu.
Iwapo unapata tatizo hili la constipation, unaweza kujaribu kunywa maji zaidi, kula milo midogo mara kwa mara, kuongeza kiasi cha nyuzinyuzi katika milo hiyo na kufanya mazoezi. Ikiwa unajitahidi kufanya hivo lakini tatizo la kupata choo kigumu au kukosa choo kabsa lipo pale pale ongea na wataalam wa afya wanaweza kukuagiza dawa za kulainisha kinyesi chako na kukusaidia upate choo vizuri. au kwa Ushauri Zaidi na Tiba juu ya tatizo lolote Tuwasiliane hapa hapa ndani ya afyaclass kupitia namba +255758286584.
4. Hali ya Braxton-Hicks contractions;
Hii ni aina ya mikazo ambayo mara nyingi hutokea kwenye kipindi cha third trimester, mikazo hii imepewa jina la Braxton-Hicks contractions, Na wakati inatokea husaidia kulainisha mlango wa uzazi( Tunasema it helps to soften the cervix). Hapa unaweza kupata maumivu ya Chini ya Kitovu.
Kumbuka; Ukiwa katika hali hii,kunywa maji mengi zaidi,badilisha mkao na usilale kifudifudi ila lala ubavu hasa ubavu wako wa kushoto, na Pia unashauriwa kupata muda wa kupumzika.
5. Mimba kukua(Pregnancy growth);
Mtoto anapokua mkubwa katika trimester ya pili na ya tatu, unaweza kupata maumivu zaidi katika eneo la chini la tumbo,kitovu na kibofu. Unaweza kuhisi hali ya ngozi yako kunyooshwa na kupata shinikizo zaidi kutoka kwa uzito ulioongezwa.
Hivo kadri mtoto anavyokuwa,uzito zaidi huongezeka eneo hili, tumbo kuongezeka ukubwa, misuli,ligaments na ngozi kwa ujumla huvutwa zaidi, na mgandamizo kuongezeka zaidi eneo hili, Hivi vyote huweza kupelekea maumivu ya chini ya kitovu,kibofu,maumivu ya kiuno pamoja na mgongo.
Hizo ni baadhi ya Sababu za kawaida za Mjamzito kupata maumivu chini ya kitovu, lakini je unafahamu zipo Sababu za hatari ambazo huweza kupelekea maumivu ya chini ya kitovu kwa mjamzito? Tuzitazame Sababu hizo;
Sababu za hatari zinazopelekea maumivu ya chini ya kitovu kwa mjamzito
Kama nilivyosema,Sababu nyingi tulizokwisha kuzitaja hapo ni za kawaida kwa Mjamzito,lakini zipo Sababu za maumivu ya chini ya kitovu au tumbo ambazo sio za kawaida kwa Mjamzito au kwa lugha nyingine hizi ni Sababu ambazo huashiria tatizo la kiafya na zinaonyesha kwamba kuna kitu hakipo Sawa.
Hizi hapa ni baadhi ya Sababu za hatari zinazoweza kusababisha maumivu ya Chini ya kitovu kwa Mjamzito;
1. Maambukizi au magonjwa mbali mbali(Infections or diseases)
Hapa nazungumzia maambukizi na magonjwa kama vile;
- Ugonjwa wa UTI;Urinary tract infection
- Tatizo la mawe kwenye Figo;kidney stones
- Tatizo la mawe kwenye kifuko cha nyongo;gallstones
- Tatizo la kuvimba kwa bandama
- Tatizo la Appendix
- Kuwa na Vidonda vya Tumbo
- Tatizo la Mzio dhidi ya vyakula mbali mbali
- Tatizo la maambukizi ya bacteria kwenye via vya uzazi;PID
- Maambukizi ya magonjwa ya Zinaa n.k
2. Kuwa na Uvimbe kwenye Kizazi
Wakati mwingine hali ya maumivu makali ya tumbo au chini ya kitovu huweza kusababishwa na Kuwepo kwa Uvimbe kwenye kizazi.
3. Tatizo la Mimba kutishia kutoka au Mimba kutoka(miscarriage)
Unaweza kuwa kwenye hatari ya mimba kutoka au kutishia kutoka, na hapa ndipo dalili mbali mbali huweza kujitokeza ikiwemo;
- Kuvuja damu nyingi ukeni
- Kupata maumivu makali ya tumbo au chini ya kitovu
- Kupata maumivu makali ya mgongo n.k
4. Tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi(Ectopic pregnancy)
Baadhi ya Tafiti zinaonyesha;Takriban mimba 1 kati ya kila mimba 50 hutunga nje ya kizazi. Huu ndio wakati yai lililorutubishwa linaposhikamana au kujishikiza sehemu ya nje na uterasi.
Ikiwa tatizo la mimba kutunga nje ya Kizazi limetokea,baadhi ya dalili mbali mbali na Ishara huweza kujitokeza,hii ni pamoja na;
- Kupata maumivu makali sana ya tumbo,chini ya kitovu,kiuno au nyonga,mgongo n.k
- Pia baadhi ya wanawake maumivu haya huweza kufika mpaka kwenye mabega na shingoni
- Kuvuja damu Ukeni
- Kupata hali ya kizunguzungu au kuzimia n.k
5. Kupata Uchungu kabla ya wakati wake(Preterm labor)
Takriban robo moja ya leba zote za kabla ya wakati (zinazotokea kabla ya wiki 37) hutokea zenyewe. Na Baadhi ya sababu za leba kuanza kabla ya wakati ni pamoja na:
- Mlango wa uzazi kuwa dhaifu( weakeness in cervix)
- Chupa kupasuka mapema
- Kupata shinikizo la juu la Damu
- Kuvuja damu wakati wa Ujauzito n.k
Hali hii huweza kusababisha mama mjamzito kuanza kupata maumivu ya chini ya kitovu au maumivu ya tumbo.
6. Tatizo la kifafa cha mimba Preeclampsia and eclampsia
Tatizo hili huhusisha shinikizo la damu kuwa juu pamoja na uwepo wa proteins kwenye mkojo. Mwanamke Mjamzito yupo kwenye hatari ya kupata kifafa cha mimba ikiwa;
- Ana shida ya shinikizo la juu la damu(High blood pressure)
- Ana ugonjwa wa kisukari
- Mnene kupita kiasi
- Kabeba mimba kwenye umri mdogo sana au kabeba mimba kwenye umri mkubwa zaidi n.k
Moja ya Dalili ambazo huweza kujitokeza ikiwa una tatizo hili ni pamoja na;
- Kupata maumivu makali ya kichwa
- Kuona marue rue
- Kupata maumivu ya tumbo
- Kuvimba sana miguu,uso,mikono n.k
7. Tatizo la Placental abruption
Tatizo hili huhusisha kondo la nyuma au placenta kuachia sehemu lilipojishikiza, na hapa dalili mbali mbali huweza kujitokeza ikiwemo;
- Mama mjamzito Kuanza kupata maumivu makali ya tumbo,chini ya kitovu na mgongo ghafla
- Kuanza kutokwa na damu nyeusi ukeni n.k
Kumbuka; Hakikisha unaongea na Wataalam wa afya ikiwa una Dalili zozote ambazo huzielewi wakati wa Ujauzito wako, ikiwemo;
✓ Kuvuja damu Ukeni
✓ Unapata Homa
✓ Unahisi maumivu wakati wa kukojoa
✓ Unapata maumivu makali sana ya tumbo au chini ya kitovu
✓ Unatokwa na Uchafu wenye rangi na harufu mbaya
✓ Unapata maumivu makali ya kichwa,kuona marue rue,kuvimba sana miguu,mikono,uso n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.