CHUCHU ZA WATOTO(Vifaa vya kumlishia Mtoto)
Hapa nazungumzia chuchu za watoto,yaani vifaa vile vya kuweka maziwa na kumpa mtoto wako, kama kwenye picha hapo.
Kwanini mada hii? Wakina mama wengi wanajisahau kwenye usafi wakati wa unyonyeshaji.
Chuchu hizi hazisafishwi vizuri, hali ambayo hupelekea mtoto kunyonya maziwa pamoja na uchafu uliopo kwenye chuchu,
na matokeo yake mtoto anaanza kulia tu, tumbo linauma, anaharisha n.k
ZINGATIA HAYA WAKATI WA UNYONYESHAJI
- Mama unayenyonyesha hakikisha mwenyewe unakuwa safi kuanzia matiti yako mpaka mwili mzima, hivo oga au nawisha matiti yako kabla ya kuanza kumnyonyesha mtoto
- Hakikisha vifaa au vyombo vyote unavyotumia kumnyonyeshea mtoto wako ni safi kabsa, kuanzia chuchu za watoto n.k
- Mnyonyeshe mtoto kwa muda unayotakiwa,sio unamnyonyesha mtoto dakika mbili halafu unakimbia,
Wengine wanasema maziwa yanatoka mepesi,
Kumbuka; maziwa ya mama yamegawanyika kwenye sehemu kuu tatu,
(i) Sehemu ya kwanza ni mepesi sana kama maji, lengo ni ili kukata kiu ya mtoto, kwani mtoto hatakiwi kunywa maji
(ii) Sehemu ya pili yanaanza kubadilika kidogo tofauti na ya mwanzo
(iii) Na sehemu ya tatu ndyo maziwa mazito, haya ndyo mtoto akiyafikia na kunyonya hushiba sasa vizuri kama chakula, ukimnyonyesha mtoto dakika mbili huwezi kuyakuta haya maziwa mazito, ambayo ndyo chakula cha kumshibisha mtoto wako.
- Unyonyeshaji wa maziwa ya mama peke yake bila mtoto kuchanganyiwa na vitu vingine vyovyote unaenda mpaka miezi sita, hii kwa kitaalam hujulikana kama EXCLUSIVE BREASTFEEDING.
- Baada ya mtoto kunyonya maziwa ya mama peke yake ndani ya miezi sita ya kwanza ndyo unaanza kumchanganyia na vitu vingine,
ila usiache kumnyonyesha mpaka afikishe miaka 2 au wengine hadi 3 kama unaweza
KUMBUKA;
• Maziwa ya mama ni kinga bora kwa mtoto wako dhidi ya magonjwa mbali mbali, hasa katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ambapo kinga ya mtoto ni ndogo saana
• Usafi wa vyombo vya kumlishia mtoto pamoja na wewe mwenye ni muhimu sana.
• Hakikisha mtoto anapata chanjo zote ikiwemo chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kifua kikuu maarufu kama BCG, chanjo ya POLIO n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.