Benjamin yafanya matibabu ya moyo kwa kutumia mshipa wa mkono kwa mara ya kwanza.
Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imefanya uchunguzi wa moyo kwa mgonjwa kwa kutumia mshipa wa mkono kwa mara ya kwanza.
Kwa mujibu wa Mkuu wa kitengo cha maabara maalum ya uchunguzi wa Moyo(Catheterization Laboratory -CathLab) cha Hospitali hio, Dkt Kelvin Masava, uchunguzi na matibabu kwa njia hio mbali na kuwa na faida nyinginezo lakini inampunguzia mgonjwa muda wa kukaa hospitalini.
“Mgonjwa anarejea kwenye shughuli zake kwa wepesi na haraka ikilinganishwa na njia ya kupitia kwenye mshipa wa mguuni tuliyokuwa tukitumia wakiitumiaa awali,” anasema
Anafafanua kuwa utaratibu huu unamuwezesha mgonjwa kunyanyuka na kutembea mwenyewe mara tu baada ya kupata huduma tofauti na apo awali.
“Njia ya mshipa wa mguuni ilihitaji mgonjwa kukaa si chini ya saa sita baada ya huduma pasipo kuinuka kitandani au kukunja mguu tofauti na hii ambapo anainuka kutembea mwenyewe na baada ya saa chache anaweza kuruhusiwa kwenda nyumbani siku hiyo hiyo,” ameongeza. @wizara_afyatz
Tumeokoa maisha ya watu wengi waliopatwa na tatizo la kupoteza mapigo ya moyo (cardiac arrest)-Benjamin Mkapa.
IDARA YA MAGONJWA YA DHARURA YA BMH YATIMIZA MIAKA MITANO
Idara ya Magonjwa ya Dharura (EMD) ya Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imetimiza miaka mitano ya huduma leo.
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura wa BMH,Dkt George Dilunga, amesema Idara hiyo imekuwa ikikuwa na kuongezeka katika utoaji huduma mwaka hadi mwaka. Idadi ya wateja wanaohudumiwa na Idara ya Magonjwa ya Dharura imeongezeka kutoka wateja 1000 kwa mwezi miaka mitano iliyopita mpaka 3500 kwa sasa.
“Tumeokoa maisha ya watu wengi waliopatwa na tatizo la kupoteza mapigo ya moyo (cardiac arrest),” amesema.
Amesema EMD itaendelea kutoa huduma mbalimbali ikiwemo uokozi katika majanga kama ajali na mafuriko yanayotokeaa sehem mbalimbali nchini.
“EMD ya BMH ilikuwa ni miongoni mwa watoa huduma waliowahi kwenda kutoa huduma Manyara kulipotokea maporoko ya tope yaliyosababishwa na mvua kubwa mwaka jana,” amesema Dkt Dilunga.
Aidha amebainisha kuwa kuna mipango endelevu ya kuhakikisha kuwa huduma bora na za wakati zinaendelea kutolewa idarani hapo ikiwemo kuhakikisha wagonjwa hawakawii kupata huduma za dharura.
Vilevile amebainisha kuwa mipango mingine endlevu ipo kuhakikisha wataalamu zaidi wa magonjwa ya dharura wanapatikana na kupewa mafunzo ili kuendelea kutoa huduma zilizo bora.
“Tuna mpango pia wa kuendeleza huduma za ambulance (EMS) pamoja na kuweka mfumo mzuri wa uokozi wagonjwa wanaopata dharura za kupoteza mapigo ya moyo (cardiac arrest) wawapo hospitalini ujulikanao kama Code Blue” alimalizia Dkt. Dilunga. @wizara_afyatz