Mkenya avunja rekodi kwa kufundisha somo la Sayansi kwa saa 62.
• • • • • •
Mwalimu kutoka Kenya Rose Tata Wekesa ameweka jina lake katika vitabu vya historia kwa kufundisha darasa refu zaidi la sayansi kuwahi kutokea, akitumia saa 62 dakika 33 na sekunde 34.
“Nina timu nyuma yangu ambayo imesaidia katika kuandaa somo. Siku tatu zilizopita, nilikesha kwa saa 44 ili kuuzoesha mwili wangu kukesha,” alisema.
Rose Tata Wakesa mwalimu katika shule ya St Austin’s Lavington amefanya jaribio hilo ikiwa ni katika hatua za kuvunja rekodi ya dunia ya Guiness kama somo lililofundishwa kwa muda mrefu zaidi.
–
Guinness World Record, bado haijaidhinisha mafanikio ya Wekesa.