Mwanamke mmoja wa Nigeria ambaye bado hajatambuliwa jina lake amekamatwa katika jimbo la Lagos nchini Nigeria kwa madai ya kuharibu gari la dereva wa Uber ambaye gari lake walipanda yeye na rafiki yake.
Katika video iliyokuwa ikizunguka, mwanaume mmoja aliyerekodi alidai kuwa mwanadada huyo aliharibu kioo cha mbele cha gari la dereva wa Uber na pia kuharibu dirisha la upande wa dereva.
Mwanamke huyo alionekana akiwa chini akiwa amewashika vyombo vya usalama walioingia kati. Alipoombwa aingie ndani ya gari ili wampeleke katika kituo cha polisi cha Maroko ambako angewasilisha malalamishi yake, Mwanamke huyo alikataa na kulazimika kuingia ndani ya gari hilo na maafisa wa usalama.
Mwanaume aliyerekodi video hiyo alidai kuwa mwanadada huyo alikuwa amelewa na dawa za kulevyia.