kadi ya kliniki ya mama mjamzito
Katika Makala hii tumefanya uchambuzi kuhusu kadi ya kliniki ya mama mjamzito,na kukusaidia kuelewa mambo mbali mbali kwenye kadi hii.
Kila mama mjamzito anapoanza kliniki kwenye hudhurio lake la kwanza,lazima apatiwe "kadi ya Kliniki ya mama mjamzito" kwa ajili ya kufwatilia maendeleo ya ujauzito wake mpaka atakapojifungua,
Kumbuka: Kuna kadi za aina mbili,ambazo ni;
- Kadi ya kliniki ya mama mjamzito
- Pamoja na Kadi ya kliniki kwa ajili ya Mtoto
Ingawa,Katika Makala hii tumechambua baadhi ya Vitu ambavyo ni muhimu sana kwenye kadi ya kliniki ya Mama mjamzito.
Uchambuzi Wa Kadi Ya Kliniki Ya Mama Mjamzito
SEHEMU ZA KADI YA KLINIKI YA MAMA MJAMZITO
1. Hapa kuna vipengele vya mwazo kabsa ambavyo huanza na taarifa muhimu za mama mjamzito(demographic data) pamoja location au sehemu ambapo mama mjamzito huyu ameanza kliniki, bila kusahau taarifa za mume wake au mwezi
- Jina la Kliniki unapoanza mahudhurio yako
- Jina la Mama Mjamzito
- Umri wa mama mjamzito
- Kimo chake au urefu wake(katika cm)
- Elimu ya mama mjamzito
- Kazi ya mama mjamzito
- Jina la Mume au mwezi
- Umri wa mume au mwezi
- Elimu ya mume au mwezi
- Kazi ya mume au mwezi
- Kijiji,mtaa au kitongoji unapotoka
- Jina la mwenyekiti
- Namba ya uandikishaji
- Namba ya hati punguzo ya chandarua
2. Habari au taarifa muhimu kuhusu Uzazi uliotangulia kwenye Kadi ya kliniki ya mama mjamzito
Hapa kuna taarifa mbali mbali za muhimu sana kuhusu historia yako ya uzazi au ujauzito uliotangulia, na taarifa hizo ni kama vile;
- Hii ni Mimba yako ya Ngapi
- Umezaa Mara ngapi
- Watoto walio hai ni wangapi
- Idadi ya Mimba zilizoharibika
- Mwaka gani mimba imeharibika
- Umri wa mimba ilipoharibika
- Tarehe ya Kwanza ya hedhi yako ya mara ya Mwisho-First date/day of last normal menstrual period(LNMP)
- Tarehe ya Matarajio ya Kujifungua-Expected date of delivery(EDD)
3. Vidokezo vya Kuchunguza kwa wajawazito wanapofika kliniki kwa mara ya kwanza(Kadi ya kliniki ya mama mjamzito);
Na hapa kila kibox kinawekewa tick kulingana na taarifa za wajawazito
- UMRI wa Mama Mjamzito;Umri wa chini ya Miaka 20 au Zaidi ya Miaka 20
- Ulijifungua Lini?:Miaka 10 au Zaidi toka Mimba ya Mwisho
- Njia ya Kujifungua;Je ulijifungua kwa njia ya Upasuaji au Kawaida
- Uhai: Kuzaa Mtoto mfu, au mtoto kufariki ndani ya wiki 1 Baada ya kujifungua.
- Mimba kuharibika; Kuharibika kwa mimba 2 au Zaidi
- Magonjwa;
- Je Una Ugonjwa wa Moyo
- Ugonjwa wa Kisukari
- Au ugonjwa wa Kifua kikuu
4. Taarifa Zaidi Za Wajawazito kwenye kadi ya kliniki ya mama mjamzito, TAARIFA HIZI HUWEZA KUONYESHA Umuhimu zaidi ya mama kupelekwa kituo cha afya au hospitalini wakati wa Kujifungua,
- Hii ni mimba yako ya 5 au Zaidi
- Una urefu wa Kimo cha chini ya cm 150
- Una shida ya Kilema cha Nyonga
- Mimba ya kwanza zaidi ya Miaka 35
- Kuzaa kwa Upasuaji au kwa Usaidizi wa vifaa kama vacuum wakati wa kujifungua
- Kutoa Damu nyingi baada ya kujifungua(Tatizo la postpartum hemorrhage-PPH)
- Tatizo la Kondo la Nyuma kukwama,
Kama mama mjamzito ana vitu hivi,hakikisha anajifungulia Hospitalini
5. VIPIMO MBALI MBALI kwenye Kadi ya kliniki ya mama mjamzito, Ikiwemo;
- Kipimo cha Wingi wa Damu
- Kundi au group la Damu pamoja na hali ya rhesus factor(POSITIVE AU NEGATIVE), kumbuka hiki ni kipimo muhimu ambacho kitatoa majibu kuhusu uchomaji wa sindano ya anti-D
- Kipimo cha Ugonjwa wa kaswende(Syphilis)
- Vipimo vya Malaria(MRDT)
- Kipimo cha Presha
- Kupima uwepo wa Proteins kwenye Mkojo
- Kupima Urefu
- Kupima Uzito
- Kupima hali ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi(VVU) N.K
6. Pamoja na Vitu Vingine kwenye Kadi ya kliniki ya mama mjamzito kama vile;
- Kuangalia hali ya Miguu kuvimba
- Hali ya Joto la mwili
- Mapigo ya Moyo kwa mama
- Mapigo ya moyo kwa Mtoto(Fetal heart rate), N.K
Hitimisho
Kadi ya kliniki ya mama mjamzito ina vipengele mbali mbali ikiwemo; kipengele cha taarifa za awali za mama mjamzito pamoja na mwenza wake(Demographic data),
Taarifa kuhusu hali ya Ujauzito uliopita,Pamoja na mambo muhimu kwenye ujauzito wa sasa, bila kusahau tarehe ya Matarajio ya kujifungua,Vipimo mbali mbali n.k
Kumbuka,Kadi ya kliniki ya mama mjamzito,ndyo huweka records au kumbukumbu ya Taarifa zote muhimu za ujauzito.