#PICHA; Wanawake wakikimbia milio ya bunduki HaitiPicha: Odelyn Joseph/AP Photo/picture alliance.
Takribani wanawake wajawazito 3,000 nchini Haiti, wanakabiliwa na kitisho cha ukosefu wa huduma za afya, wakati hali ya kibinadamu katika mji mkuu wa Port-au-Prince ikiendelea kuzorota.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Haiti, imeonya jana kwamba karibu wanawake 450, huenda wakakabiliwa na matatizo ya uzazi ambayo yanatishia maisha ikiwa hawatapokea msaada wa matibabu.
Mgogoro wa Haiti umeibua wasiwasi kutoka kwa Marekani ambayo imemtaka waziri mkuu wa nchi hiyo, aliyeko nchi jirani kufanya mageuzi ya haraka ya kisiasa ili kuzuia kuongezeka zaidi kwa ghasia.
Makundi ya wahalifu, ambayo tayari yanadhibiti sehemu kubwa ya mji mkuu pamoja na barabara zinazoelekea katika maeneo mengine ya nchi, yameshambulia miundombinu muhimu katika siku za hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na magereza mawili, na kuruhusu wafungwa zaidi ya 3,000 kutoroka.