Sababu ya mashavu ya uke kuwasha
Baadhi ya Wanawake hupatwa na tatizo la mashavu ya uke kuwasha lakini hawajui shida hii imetokana na nini?
Katika Makala hii tumekuchambulia baadhi ya Sababu za mashavu ya uke kuwasha, Soma Zaidi hapa…!!!!
Chanzo cha mashavu ya uke kuwasha
Hizi hapa ni baadhi ya Sababu za mashavu ya uke kuwasha;
1. Maambukizi ya Fangasi(Yeast infections)
Wanawake wengi hushambuliwa na fangasi sehemu za Siri(candida albicans), hali ambayo hupelekea kupata dalili mbali mbali ikiwemo;
- mashavu ya uke kuwasha
- Kuhisi kuungua ukeni
- Kutoa uchafu mweupe kama maziwa mgando ukeni n.k
2. Tatizo la Bacterial vaginosis
Bacterial vaginosis (BV) ni tatizo linalohusisha maambukizi ya bacteria Ukeni,
Hutokea pale ambapo hakuna uwiano sawa kati ya bacteria wazuri wa Ukeni, Wanawake wenye tatizo hili huweza kupata dalili mbali mbali ikiwemo;
- mashavu ya uke kuwasha(nje)
- Kuwashwa ndani ya Uke
- Kupata maumivu ukeni
- Kuhisi hali ya kuungua ndani ya uke
- kutokwa na uchafu mwembamba mweupe au kijivu ukeni
- Kutoa harufu mbaya ukeni hasa baada ya tendo n.k
3. Matatizo ya ngozi(Skin conditions)
Mashavu ya uke kuwasha huweza kusababishwa na matatizo ya ngozi kama vile;
- Tatizo la psoriasis
- seborrheic dermatitis
- Tatizo la Mzio au allergy kwenye ngozi(allergic contact dermatitis)
- folliculitis
- dermographism/ skin writing n.k
Pia mashavu ya uke kuwasha sana inaweza Kuashiria tatizo la lichen sclerosus au ichen planus.
4. Magonjwa ya Zinaa
Tatizo la Mashavu ya uke kuwasha huweza kusababishwa na Magonjwa ya Zinaa, hapa tunazungumzia magonjwa ya Zinaa kama vile;
- genital herpes
- Pamoja na trichomoniasis
5. Tatizo la masundosundo(genital warts)
Baada ya Mwanamke kupata tatizo la genital warts kutokana na maambukizi ya kirusi cha Human papilloma Virus(HPV) anaweza pia kukumbana na tatizo la mashavu ya uke kuwasha.
6. Tatizo la maambukizi ya Bacteria kwenye Via vya Uzazi vya Mwanamke(PID)
Ugonjwa wa PID pia unaweza kuchangia tatizo la mashavu ya uke kuwasha.
7. Sababu Zingine…!!!!
Ingawa ni mara chache kutokea lakini matatizo kama vile;
(i) Saratani ya Mashavu ya Uke(Vulvar cancer) huweza kusababisha mashavu ya uke kuwasha,
Aina hii ya Saratani ni adimu sana kutokea, na dalili zake ni pamoja na;
- mashavu ya uke kuwasha
- Kuhisi kuungua kwenye mashavu ya uke
- Kuvuja damu n.k
(ii) Pia Tatizo la uharibifu wa neva(Neuropathy), huweza kusababisha mashavu ya uke kuwasha
8. Miwasho kutokana na matumizi ya baadhi ya Vitu
Wakati mwingine tatizo la mashavu ya uke kuwasha huweza kutokana na matumizi ya vitu vinavyotuzunguka kama vile;
- Baadhi ya Pedi(menstrual pads)
- Baadhi ya Materials kwenye nguo za ndani
- chupi zilizofuliwa na sabuni zenye harufu nzuri ila zina kemikali flani ndani yake
- Baadhi ya Sabuni za kuogea
- Baadhi ya Mafuta ya Kupaka,lotions au creams n.k
- Matumizi ya kondoms(latex condoms)
- Manukato ndani ya deodorants n.k
Na hapa; Kuwashwa kwenye Mashavu ya Uke kwa kawaida kutaisha baada ya mtu kuacha kutumia bidhaa hizi.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.