CHANZO CHA TATIZO LA KUKOJOA MKOJO MWEUSI
Chanzo cha tatizo la kukojoa mkojo mweusi huweza kuhusisha sababu nyingi kidogo na kuondoa zile imani za baadhi ya watu kwamba kukojoa mkojo mweusi ni kulogwa, lahasha! hii ipo kitaalam kabsa na kuna sababu mbali mbali za kutokea kwa hali hii ya rangi ya mkojo kubadilika na kuwa nyeusi.
SABABU ZA RANGI YA MKOJO KUBADILIKA NA KUWA NYEUSI WAKATI WA KUKOJOA NI PAMOJA NA;
1. Mtu kuwa na upungufu mkubwa wa maji mwilini yaani dehydration, hali hii huweza kusababisha mtu kukojoa mkojo mweusi, Kukauka mdomo,lips, Kuwa na kiu ya maji kupita kiasi,kupatwa na kizunguzungu,kujisaidia choo kigumu sana,mwili kuchoka kupita kiasi n.k
Unashauriwa kunywa maji kila siku angalau lita 2.5 mpaka 3 za maji kwa masaa 24, hii itakusaidia wewe kuwa na afya bora na kujikinga na magonjwa mbali mbali kama vile UTI n.k
2. Ulaji wa baadhi ya vyakula pamoja na vinywaji huweza kusababisha pia rangi ya mkojo kubadilika na kuwa nyeusi, mfano matumizi ya Beets pamoja na Blackberries huweza kubadilisha kabsa rangi ya mkojo wakati unakojoa.
3. Matumizi ya baadhi ya Dawa, kuna dawa mbali mbali ambazo huweza kusababisha tatizo la rangi ya mkojo kubadilika na kuwa nyeusi kama vile; matumizi ya Dawa jamii ya Chlorpromazine,warfarin,
phenazopyridine,Rifampin,chloroquine n.k
4. Tatizo la Hemolytic anemia,ambapo seli nyekundu za damu yaani Red blood cells(RBC's) huharibiwa kwa kiwango kikubwa sana, hali hii huweza kusababisha mtu kupatwa na dalili mbali mbali kama vile; Kukojoa mkojo wenye rangi Nyeusi, maumivu makali ya kichwa,kupatwa na kizunguzungu,homa,rangi ya ngozi kwenye Lips,mikono, machoni kuwa nyeupe kuliko kawaida n.k
5. Maambukizi ya Bacteria kwenye mfumo wa mkojo yaani UTI, endapo bacteria wameshambulia na kuingia kwenye kibofu cha mkojo huweza kusababisha tatizo la mtu kukojoa mkojo wenye rangi nyeusi,maumivu makali wakati wa kukojoa, kuhisi kuungua wakati wa kukojoa,kukojoa mara kwa mara n.k
6. Tatizo la Hepatitis C, mbali na virusi vya Hepatitis B ambapo wengi huvisikia sana, kuna mashambulizi ya virusi vys Hepatitis C pia ambao hujulikana kama Hepatitis C Virus(HCV), Hawa pia huweza kusababisha tatizo la mtu kukojoa mkojo wenye rangi nyeusi baada ya kuanza mashambulizi yake kwenye Ini, pamoja na mgonjwa kupatwa na dalili zingine kama vile; kuchoka sana au kupita kiasi,kupata maumivu kwenye joints,joto la mwili kupanda sana au mtu kuwa na homa kali, kuhisi kichefuchefu mara kwa mara,kukosa kabsa hamu ya kula,maumivu makali ya tumbo,mwili kuanza kuwasha sana n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.