TATIZO LA KUOTA MVI MAPEMA
Tatizo hili lipo kwa watu wengi tu siku hizi huku tafti zikionyesha baadhi ya Sababu mbalimbali ambazo huleta tatizo hili la Kuota Mvi Mapema.
Baadhi ya Sababu Hizo ni Pamoja na;
1. Sababu ya Kijenetiki.
Ukweli ni kwamba kuna baadhi ya watu huota mvi mapema kutokana na kurithi baadhi ya Genetics hizo kutoka katika Familia husika. Tatizo la nywele kubadilika rangi mapema huweza kulipata katika koo,Mfano baba, Mjomba n.k
2. Ukosefu wa Virutubisho vya Vitamin Mwilini.
Ukosefu wa virutubisho vya Vitamin kama vile Vitamin B12 huweza kusababisha rangi ya nywele kubalika Mapema. Vitamin hivi kupatikana katika vyakula mbalimbali kama Nyama ya Ng'ombe,Mayai n.k
3. Tatizo katika Vichocheo vya mwili.
Shida katika tezi (Thyroid gland) katika kuzalisha vichocheo hasa kichocheo cha Melanin ambacho huleta rangi katika ngozi, huweza kusababisha kubalika kwa rangi ya nywele, hivo kupelekea kuwa na tatizo la kuota Mvi mapema
4. Maradhi yanayosababisha mwiitiko usio wa kawaida wa Seli za kinga ya mwili.
Shida hyo husababisha seli zenyewe kushambuliana hivo,kupelekea seli za kinga ya mwili kuathiri zile zinazozalisha Melanin.Kama vile kwa mtu aliyepatwa na shida ya Vitiligo
5. Matumizi ya rangi na dawa mbalimbali za nywele.
Hapa tunazungumzia hasa hasa dawa zenye kemikali za hydrogen perioxide huweza kusababisha tatizo hili la kuwa na Mvi mapema
6. Uvutaji wa Sigara.
Watu wengi hawajui kwamba Sigara zina madhara mengi sana mwilini,mbali na magonjwa kama ya Moyo,mapafu,kansa n.k, Bali pia kemikali zilizopo ndani ya sigara huweza kusababisha rangi ya nywele kubadilika.
TIBA
Ukweli ni kwamba hakuna matibabu ya tatizo hili,isipokuwa tu kuficha mvi zisionekane kama kwa kupaka vitu kama piko, lakini sio kuzitibu.