AFYA YA UZAZI
• • • •
Sababu za Mimba Kutunga Nje ya Kizazi pamoja na Dalili zake(Ectopic pregnancy)
Kwa asilimia kubwa Mimba kutunga Nje ya kizazi yaani kwa kitaalam Ectopic pregnancy hutokea wakati yai lililorutubishwa kukwama ndani ya mirija ya uzazi(fallopian tubes) au kuelekea kwenye njia ya uzazi, japo mimba kutunga sehemu nyingine yoyote mbali na sehemu yake ya kawaida ndani ya kizazi bado ni Ectopic pregnancy,
CHANZO CHA TATIZO HILI LA MIMBA KUTUNGA NJE YA KIZAZI
- mara nyingi mimba hutunga nje ya kizazi kwa sababu mirija ya uzazi yaani fallopian tubes imeharibiwa, kuziba au kufungwa vibaya.
- Tatizo la mvurugiko wa vichocheo mwilini(hormone imbalance) au ukuaji usiokuwa wa kawaida wa yai lililorutubishwa pia linaweza kuchangia tatizo hili.
• Vitu vingine ambavyo vinaweza kuchangia tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi ni pamoja na:
✓ Kuwa na tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi kwenye ujauzito wa nyuma. Ikiwa umewahi kuwa na ujauzito wa aina hii hapo awali, una uwezekano mkubwa wa kuwa na mwingine.
✓ Uvimbe au maambukizi ya magonjwa mbali mbali. Maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama; kisonono au chlamydia, yanaweza kusababisha kuvimba kwenye mirija na viungo vingine vya karibu, na kuongeza hatari ya ujauzito kutunga nje ya kizazi(ectopic pregnancy).
✓ Matibabu kwa ajili ya kupata mtoto. Utafiti mwingine unaonyesha kwamba wanawake ambao wamewahi kufanyiwa In- Vitro fertilization (IVF) kwa ajili ya kupata watoto au matibabu kama hayo wana uwezekano wa kuwa na tatizo la ujauzito kutunga nje ya kizazi(ectopic pregnancy).
Pia kukaa kwa muda mrefu sana bila kuzaa au kuzaa mapema sana huweza kuongeza uwezakano wa tatizo
✓ Upasuaji katika mirija ya uzazi(Tubal surgery). Upasuaji wa kurekebisha tatizo lolote kwenye mirija ya uzazi yaani fallopian tubes huongeza hatari ya Mwanamke kupatwa na tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi.
✓ Aina ya njia ya uzazi wa mpango ulioichagua. Uwezekano wa kupata ujauzito wakati unatumia kifaa kama intrauterine device (IUD) ni mdogo sana.
Lakini endapo kwa bahati mbaya ikitokea umebeba mimba na una kifaa cha IUD ndani yako, uwezekano wa mimba kutunga nje ya kizazi ni mkubwa.
Njia ya kufunga uzazi(Tubal ligation), njia hii ni ya kudumu ya kudhibiti uzazi lakini ikiwa utapata ujauzito baada ya utaratibu huu uwezekano wa mimba hyo kutunga nje ya kizazi ni asilimia 100.
✓ Uvutaji sigara. Uvutaji sigara kabla tu ya kupata ujauzito unaweza kuongeza hatari ya ujauzito kutunga nje ya kizazi. Kadri unavyovuta sigara, ndivyo hatari inavyo kuwa kubwa zaidi.
DALILI ZA MIMBA KUTUNGA NJE YA KIZAZI
Huenda usione dalili yoyote mwanzoni. wanawake wengi ambao wana tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi(ectopic pregnancy) wanapata dalili zote za awali za ujauzito kama vile; kukosa period au kutokuona siku zao za hedhi, matiti kujaa, kichefuchefu N.k.
Ikiwa unapima ujauzito au mimba, matokeo yatakuwa mazuri tu kama kawaida na kuonyesha kwamba wewe ni mjamzito. Tofauti tu ni kwamba matatizo huanza kutokea pale ujauzito unavyozidi kukua.
- Mara nyingi, dalili za kwanza kabsa kama una tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi ni damu nyepesi kuanza kutoka ukeni na maumivu ya kiuno au nyonga.
Ikiwa damu huvuja kutoka kwenye mirija ya uzazi(fallopian tubes), unaweza kuhisi maumivu ya bega au hamu ya kuwa na haja kubwa. Dalili maalum hutegemea mahali damu inajikusanya na mishipa ipi inaathiriwa.
Ikiwa yai lililorutubishwa linaendelea kukua kwenye mrija wa fallopian, linaweza kusababisha mrija huo wa uzazi kupasuka. Matokeo yake ni Kutokwa na damu nzito ndani ya tumbo la uzazi. Dalili kama hii huweza kuhatarisha maisha,kusababisha maumivu makali ya kichwa, kuzimia na mshtuko.
KUMBUKA; NENDA HOSPITAL HARAKA UKIONA DALILI KAMA HIZI HAPA;
• Maumivu makali ya tumbo na kutokwa na damu ukeni
• Maumivu makali ya Kichwa au kuzimia
• Maumivu ya bega N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.