Ticker

6/recent/ticker-posts

ATHARI ZA MAGONJWA YA ZINAA KWA WAJAWAZITO



MAGONJWA

• • • • • •

ATHARI ZA MAGONJWA YA ZINAA KWA WAJAWAZITO


Magonjwa ya zinaa ni maambukizi yaenezwayo kutoka mtu mmoja hadi mwingine kwa kufanya ngono na mtu mwenye vimelea vya ugonjwa. Aina ya vimelea vinavyohusika kusababisha magonjwa haya ni kama bakteria, virusi na aina nyinginezo za vimelea vya magonjwa.


Kuna aina nyingi za magonjwa ya zinaa yanayojulikana, lakini baadhi ya hayo ni kama kisonono,  malengelenge, HIV/AIDS,Pangusa,Chlamydia, HPV(Human

Papilloma Virus),Kaswende, Trichomuniasis na mengineyo mengi.


Wanawake walio wajawazito waweza kuambukizwa magonjwa ya zinaa sawa na wanawake wasio wajawazito. Magonjwa haya ya zinaa mengi huwa hayaonyeshi dalili mtu anapoambukizwa, kwa hiyo ni vigumu wakati mwingine kwa kina mama wenye mimba kugundua kama wameambukizwa magonjwa haya.Kina mama walio wajawazito ni vyema kuhudhuria kliniki ili wafanyiwe uchunguzi wa magonjwa ya zinaa ikiwepo HIV ambayo husababisha Udhaifu wa Kinga Mwilini.


Ni vyema kina mama wajawazito kufahamu madhara ya magonjwa haya kwa afya zao pamoja na mimba inayokua tumboni. Wenza wa kina mama walio athirika ni lazima nao waudhurie kliniki kwa ajili ya vipimo na matibabu.


Magojwa ya zinaa yaweza kusababisha madhara makubwa kwa mama na mtoto. Baadhi ya madhara haya yaweza kuonekana wakati mtoto anapozaliwa, lakini madhara mengine huendelea kujitokeza baada ya miezi hata miaka mingi baadaye.


 Ugunduzi wa mapema ni muhimu kwa kuwa maambukizi mengine ya magonjwa ya zinaa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yaweza kuzuiliwa endapo itagundulika mapema, mfano  yawezekana kuzuia maambukizi ya HIV kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa kutumia dawa maalum ambazo mama hupewa wakati wa ujauzito.






Post a Comment

0 Comments