Ticker

6/recent/ticker-posts

HALI YA MTOTO KUNYONYA VIDOLE INASABABISHWA NA NINI?



KUNYONYA VIDOLE

• • • • • •

Kwanini mtoto ananyonya kidole/vidole? Mtoto anaanza kunyonya kidole ikiwa atakuwa hakupata maziwa ya kutosha, mara nyingine husababishwa na matatizo ya kihisia. Mtoto asipotosheka kila anaponyonya huanza tabia ya kunyonya kidole


Kunyonya vidole husababisha meno kutojipanga vizuri kwenye fizi. Madaktari wa kinywa wamehusisha matatizo ya kuwa na meno yasiyo jipanga vizuri na kunyonya kidole hasa kidole gumba kwani meno husukumwa kwenda mbele au kujipanga vibaya. 


Inashauriwa usimfanye mtoto aache kunyonya kidole akiwa na umri chini ya miaka 4 au 5 isipokuwa tu pale utakapoona kuna tatizo linalojitokeza kwa sababu ya kunyonya kwake kidole au ikiwa mtoto ataanza ghafla baada ya miezi 10 & ikiambatana na kuvuta nywele


Ili mtoto aache kunyonya kidole mpatie michezo ambayo itaufanya huo mkono anaonyonya wakati wote uwe na shughuli ya kufanya, kama vile acheze puzzle, achezee midoli ili mradi tu viganja vyake viwe na shughuli

 #drtareeq

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!






Post a Comment

0 Comments