Ticker

6/recent/ticker-posts

MAFUTA YA NAZI YAMETHIBITISHWA KUPAMBANA NA MASHAMBULIZI MENGI MWILINI KAMA VIRUS



NAZI

• • • • • •

MAFUTA YA NAZI YAMETHIBITISHWA KUPAMBANA NA MASHAMBULIZI MENGI MWILINI KAMA VIRUS 

Manufaa ya kutumia nazi kiafya katika mlo wako.

Nazi ni moja vyanzo vizuri vya viinilishe vingi,Fahamu umuhimu wake sasa.


1. Kupunguza uzito uliozidi.

Sote tunajua kuwa uzito uliokithiri ni hatari kwa afya kwani hushusha ufanisi Wa kinga ya  mwili karibia 50% hivyo kuufanya mwili kuwa hatiani kushambuliwa na magonjwa kwa urahisi. Nazi inamafuta yajulikanayo kama #MEDIUM_CHAIN_TRIGLYCERIDES_(MCTs), mafuta haya yanapoingia mwilini yanasifa ya kuunguzwa haraka na kutoa nishati muhimu mwilini. Husaidia kuondoa mafuta mengine mabaya mwilini ambayo hutengeneza sumu(free radicals) ambazo ni wakala wakubwa Wa kusababisha uzito na magonjwa mengine.


2. Nazi inasaidia kuimarisha mfumo Wa kinga ya mwili kwa sababu ya uwezo wake mkubwa Wa kupambana na virus,bakteria,Fangasi,na vimelea vya magonjwa.


3. Nazi huboresha mfumo Wa mmeng'enyo Wa chakula na kusaidia virutubisho kufyonzwa vizuri mwilini.


4. Nazi inauwezo mkubwa Wa kuzalisha nishati ya mwili kwa haraka sana na pia kuzuia kuwa na njaa za Mara kwa Mara.


5. Inasaidia katika utolewaji Wa homoni ya insulini ambayo hurekebisha kiwango cha sukari mwilini na kupambana na dalili zote za kisukari.


6. Nazi inaulinda mwili dhidi ya kansa/saratani kutokana na uwezo wake mkubwa Wa kuzuia kiwango cha insulini kisizidi,kuangamiza free radicals ambazo ni sumu zinazopelekea kuzeeka mapema na usambaaji Wa kansa mwilini.


7. Nazi inasaidia kulinda afya ya moyo na kuboresha uwingi Wa lehemu salama kiafya yani HDL


8. Nazi inarejesha na kusaidia Nazi za tezi ya thairod.


9. Nazi inalinda na kuzuia magonjwa kwenye Figo na kibofu cha mkojo.


10. Nazi husaidia kupunguza kasi ya kuzeeka,kuboresha afya ya nywele,ngozi,kuondoa makunyanzi,vidoti vyeusi kwenye ngozi na kukinga na mionzi ya jua.


Unaweza kutumia nazi kama maziwa,mafuta,mkate,jibini,yogurt






Post a Comment

0 Comments