Ticker

6/recent/ticker-posts

MAMA MJAMZITO KULA UDONGO(PEMBA)



 JE WAJUA PEMBA SIO NZURI?


SOMA HAPA..!!!


Kuna madhara mengi ambayo huweza kumpata mama mjamzito kwa kula Udongo maarufu kama PEMBA. Hebu tuone kwanza nini kinapatikana kwenye udongo huu ambao mama wengi wakiwa wajawazito hupendelea kula.


Chuo kikuu cha Afya na Sayansi BUGANDO wakishirikiana pamoja na Wenzetu kutoka CANADA na MAREKANI walifanya utafiti katika Mikoa 12 Ya Tanzania ambayo ni;


  1. RUVUMA
  2. TANGA
  3. KILIMANJARO
  4. KIGOMA
  5. MOROGORO
  6. MARA
  7. KUSINI PEMBA
  8. MBEYA
  9. DODOMA
  10. LINDI
  11. RUKWA
  12. SINGIDA

Majibu ya utafiti huo; Waligundua kwamba ndani ya udongo kuna madini mengi ambayo ni hatari kwa afya ya mama na mtoto aliyetumboni, madini hayo ni pamoja na;


  • Aluminium
  • Nickel
  • Cadmium
  • Arsenic
  • Pamoja na madini ya Risasi au Lead


Kumbuka pia; Mbali na utafiti huo,kwa hali ya kawaida ndani ya udongo kuna uchafu wa kila namna unaojua wewe, Kama vile kinyesi,mikojo, n.k


Epuka Tabia Hii kwa afya Bora kwako na Mtoto wako aliyetumboni.

Kinga ni Bora kuliko Tiba

WE CARE, WE SHARE...!!!!



@Kwa Ushauri zaidi,elimu au Tiba usisite pia tuwasiliane kupitia namba +255758286584.








Post a Comment

0 Comments