KINGA
• • • • • •
♣MATATIZO YATOKANAYO NA KUSHUKA KWA KINGA YA MWILI.♣
Kwa kawaida mwili wa binadamu yeyote umeumbwa na kinga ya mwili ya asili ambayo lengo lake kuu ni kuulinda mwili dhidi ya vimelea vya magonjwa.Inapotokea kimelea (vimelea) kuingia katika mwili wa binadamu kwa njia yoyote (kunywa au kula vimelea,kugusana na majimaji au ngozi ya mtu mwenye vimelea,au kupitia damu yenye vimelea n.k), mwili hutengeneza kingamwili (antibodies) ambazo hupigana na vimelea hivyo ili kuuweka mwili katika afya njema kama hapo awali.Vile vile kwenye ngozi, mfumo wa chakula, ukeni, uumeni n.k Hata hivyo vijidudu hivi huweza kuwa chanzo cha magonjwa iwapo kinga ya mwili itashuka.
Magonjwa nyemelezi ni yale ambayo hushambulia mwili wa binadamu pale uwezo wa kinga ya mwili kupigana na vimelea vya magonjwa unaposhuka.Ni magonjwa ambayo katika hali ya kawaida hayategemewi kujitokeza kwa mtu mwenye kinga kamili ya mwili.
Magonjwa nyemelezi husababishwa na vijidudu mbalimbali kama bakteria, virusi na fangasi.Baadhi ya Magonjwa hayo ni kama yafuatayo:-
Kifua kikuu
Nimonia
Maumivu ya retina
Ugonjwa wa ngozi
Ugonjwa wa malengelenge
Mkanda wa jeshi
Homa ya UTI wa mgongo
Kuugua mara kwa mara n.k
Ni wakati wetu wote tufahamu ni jinsi gani yatupasa kuimarisha kinga zetu kwa kufuata kanuni za ulaji bora na kuachana na baadhi ya tabia ambazo zitakufanya kushuka kwa kinga ya mwili. Na kama unajua kuwa kinga ya mwili wako imeshuka basi usisite kuwasiliana nasi ili uweze ushauri na ni vitu gani ufanye uweze kuimarisha kinga ya mwili wako.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!
Emoji