Ticker

6/recent/ticker-posts

TATIZO LA INFERTILITY(UGUMBA)



INFERTILITY

• • • • • •

Watu wengi hudhani kama mwanamke hapati ujauzito basi tatizo na lawama zote zitakuwa ni upande wa mwanamke, lakini hilo si lazima mara zote liwe hivyo. Kuna uwezekano mkubwa kuwa tatizo la kutopata mtoto katika familia likawa linatokana na ugumba upande wa mwanaume.


Mwanaume kuzalisha mbegu chache kuliko kawaida ni mojawapo ya sababu kubwa za ugumba kwa wanaume.


MBEGU CHACHE NI KIASI GANI?


Shahawa kawaida ni mchanganyiko wa maji maji (ute) unaotengenezwa na tezi dume na mbegu za kiume (manii). Mtu anakua na tatizo la mbegu chache pale katika kila Millilita moja ya shahawa zake kunakua na mbegu (manii) chini ya millioni 15. Kwa kawaida mwanaume anazalisha zaidi ya manii millioni 20 katika kila millilita moja ya shahawa anazomwaga.


Kitaalamu tatizo hili linaitwa OLIGOSPERMIA (ol-ih-go-spur-me-uh), na kutokuwa na mbegu za kiume kabisa kwenye shahawa inajulikana kama AZOOSPERMIA


DALILI

Dalili kuu ya tatizo hili ni kushindwa kutungisha mimba/kupata mtoto.Zinaweza kuwepo dalili nyingine kulingana na chanzo cha tatizo hili mfano mirija ya manii kuziba,matatizo kwenye korodani na matatizo kwenye mfumo wa hormone.

Dalili nyingine ni kama

Matatizo kwenye uwezo wa kufanya tendo la ndoa mfano kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa,uume kushindwa kusima au kuwa mlegevu unaposimama.

Maumivu na uvimbe kwenye korodani

Kupungua au kutokuwa na ndevu na nywele za sehemu nyingine za mwili ,hii ni dalili ya uhaba au upungufu wa hormone ya testosterone.


 VISABABISHI


Kutengenezwa kwa mbegu inahusisha korodani na tezi iliyopo kwenye ubongo inayojulikana kama hypothalmus ambayo hii inahusika na kuzalisha hormone zinazochochea uzalishwaji wa mbegu za kiume. Matatizo katika viungo hivi huweza kupelekea tatizo hili.

 Pia kuna weza kuwepo na matatizo katika maumbo ya mbegu za kiume nayo kupelekea tatizo hili.


Visabibishi vya tatizo hili ni kama ifatavyo:


SABABU ZA KIAFYA

 1.Kuvimba kwa mishipa ya damu ya korodani-Varicocele ,hali hii inaathiri kiwango cha joto kwenye korodani hivyo kuathiri utengenezwaji wa mbegu za kiume.


2.Maambukizi, Baadhi ya maambukizi yanaweza kuathiri utengenezwaji wa mbegu za kiume na jinsi mbegu hizi zinavyotelewa nje.Magonjwa ya zinaa,magonjwa ya korordani yanaweza kupelekea kuziba kwa mirija ya manii na kuharibu seli zinazohusika na kutengeneza manii kwenye korodani.


3.Matatizo katika kutoa mbegu nje mfano tatizo la misuli ya shingo ya kibofu kutobana vizuri hivyo kupelekea shahawa kuingia kwenye kibofu cha mkojo badala ya kutolewa nje.


4.Kinga ya mwili kuziharibu mbegu.Kuna tatizo la kinga ya mwili kuzisoma mbegu za kiume kama wadudu wanaoleta magonjwa hivyo kuziharibu (sperm ant bodies)


5.Saratani, kuna baadhi ya saratani kama saratani ya tezi ya pituitari,saratani ya korodani zinaathiri pia utengenezwaji wa mbegu za kiume


6.USAWA WA HOMONI USIO SAWA (Hormone Imbalance):

Tatizo la homoni kutokuwa sawa si jambo linalowapata wanawake peke yao, ni jambo linalojitokeza pia kwa wanaume ingawa wengi wao huwa hawana muda wa kufikiri kuwa nalo. Homoni zina umhimu mkubwa katika kazi ya uzalishaji wa mbegu na katika afya ya uzazi wa mwanaume kwa ujumla.


Moja ya homoni kuu inayohusika na uzazi kwa mwanaume ni homoni ya testosterone. Kutokana na maisha yetu ya kisasa na baadhi ya matatizo yaliyoelezwa hapo juu upande wa uwingi wa mbegu, wanaume wengi wanajikuta katika hali hii ya kuwa na tatizo la homoni zao kutokuwa katika usawa unaohitajika kwa afya bora ya uzazi.

Vipo vitu vinavyoweza kuharibu homoni ya testerone na huanza kwa kuigiza au kijifanya vyenyewe ni estrogens (xenohormones). Estrogen ikizidi katika mwili wa mwanaume hupelekea uhanithi (uume kushindwa kusimama), kukosa hamu ya tendo la ndoa, kupungua kwa mbegu na kupungua kwa maji maji ya mbegu kwa ujumla.


Visababishi hasa vya kuharibika kwa testeroni ni pamoja na

• Vyakula vyenye soya

• Madawa yanayotumika katika mazao mashambani

• Hormone zinazoongezwa katika bidhaa za maziwa na nyama

7.Mishipa ya manii kuziba


8.Madawa, Baadhi ya madawa mfano dawa za kutibu saratani,dawa za fangasi,na baadhi ya ant biotic zikitumika kwa muda mrefu zinaweza kusababisha tatizo hili.


9.Mfadhaiko (Stress


10.Uvutaji wa Sigara

11.Unywaji pombe – Katika moja ya utafiti kwa wanaume wenye mbegu zenye ubora wa chini, matumizi ya kupitiliza ya unywaji pombe yalionyesha kuhusika na kupungua kwa mbegu za kawaida yaani mbegu nzuri zinazofaa kwa ajili ya uzazi.


 JINSI YA KUJIKINGA


Njia kubwa ya kujikinga  na tatizo la mbegu chache ni kula vyakula vyenye virutubisho vinavyosaidia kuongeza uzalishaji na ubora wa mbegu za kiume.


Njia nyingine ni pamoja na:

kuacha kuvuta sigara

kutokunywa pombe kupindukia

kutotumia dawa za kulevya

kuepuka msongo wa mawazo

kutovaa nguo zinazobana sana korodani

kupunguza uzito uliozidi

Epuka kula vyakula vyenye Soya mfano mbegu za soya,maziwa ya soya






Post a Comment

0 Comments