Ticker

6/recent/ticker-posts

UMUHIMU WA KUPIGA ULTRASOUND KIPINDI CHA UJAUZITO



ULTRASOUND

• • • • • •

UMUHIMU WA KUPIGA ULTRASOUND KIPINDI CHA UJAUZITO 

.

Kwanza ultra sound HAINA MADHARA KABISA,haitumii MIONZI kama Xray.


Ultrasound inatumia MAWIMBI YA SAUTI yaani SOUND WAVES na kuleta picha au muonekano wa mtoto kama ni kizazi etc.


Na kazi za Ultrasound kwa mama Mjamzito ni hizi

1.kuhakiki uwepo wa mimba


2.kujua umri wa Mimba mfano mimba ina wiki ngap na kusaidia makadilio ya kujifungua yaan EDD


3.kuangalia idadi wa watoto kama ni mapacha au mmoja


4.kuangalia complications za Mimba mfano mimba imetoka au mimba imetunga nje ya kizazi....


5.Kumwangalia mtoto kama hana matatizo ya viungo yaan birthdefects mfano kichwa kikubwa na mengineyo.


6.kuangalia complication zingine za mimba mfano kuangalia kondo la nyuma kama limekaa mahali sahihi halijaachia kuangalia kama mtoto kitovu hakijazunguka shingoni..


7.Kuangalia jinsia ya mtoto.


NB: Ni muhimu mama k ambae hana tatizo lolote kupiga ultrasound Walau MBILI mpaka anajifungua na ya kwanza ni kabla mimba haijafika Wiki 14 nyingine ni mimba ikiwa kubwa mwishon mwishon ili kuangalia maendeleo ya mtoto 


Na wamama wajawazito wengine hupiga ultrasound nyingi sana hata zaidi ya 6 kutokana na complications walizo nazo...


Na sehemu zilizoendelea zaid zenye huduma nzuri  kila clinic mama  K unafanya ultrasound kujua tu Mtoto anaendeleaje, mapigo ya moyo, kilo zake, alivyokaa..


Eheee mama k,umepiga ngap mpaka sasa?????






Post a Comment

0 Comments