Ticker

6/recent/ticker-posts

WANAUME WENGI WAMEKUWA WAKIHISI KUWA WANA MATATIZO YA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME



NGUVU ZA KIUME

• • • • • •

Wanaume  wengi wamekuwa wakihisi kuwa wana matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na kwamba wanahitaji tiba ya dawa kumbe tatizo ni wasiwasi wao katika kipindi cha kufanya tendo la ndoa. 


Tatizo la wasi wasi wakati wa kufanya tendo la ndoa huwapata wanaume wengi na kujikuta wanashindwa kumudu tendo hilo.

Ili uweze kujua kwamba wewe ni mhanga wa tatizo hili au la jiulize maswali yafuatayo:

.

1. Je, umekuwa unapata tatizo la jogoo kushindwa kuwika wakati ukiwa faragha na mpenzi wako, lakini ukiwa peke yako uume una uwezo wa kusimama kwa kujigusa mwenyewe ukiwa chumbani kwako na bila kuangalia picha za ngono?


2. Je, uume wako umekuwa ukisimama na kisha kusinyaa wakati fulani ukiwa na mwanamke na hasa pale unapokutana na mwanamke huyo kwa mara ya kwanza au ya pili?


3. Umekuwa ukipata wasiwasi kuhusu uume wako kuwa tayari utakapokutana na mwanamke?


4. Umekuwa ukikwepa kufanya tendo la ndoa kwa wasiwasi kuwa pengine utashindwa kumridhisha mpenzi wako?


Kama majibu ni ndiyo kwa baadhi au kwa maswali haya yote basi una tatizo la kushindwa kufanya tendo la ndoa kwa sababu ya kuwa na wasiwasi..






Post a Comment

0 Comments