FAHAMU FAIDA 5 ZA KUNYWA MAJI KABLA YA KULA CHOCHOTE(unapoamka asubuhi)

 MAJI YA KUNYWA

• • • • • •

FAHAMU FAIDA 5 ZA KUNYWA MAJI KABLA YA KULA CHOCHOTE(unapoamka asubuhi)


Karibu ufahamu faida 5 za msingi za kunywa maji kabla ya kula chochote unapoamka.


1. Huondoa sumu mwilini


Unywaji wa maji mengi husaidia kuondoa sumu mwilini kwani huwezesha viungo kama vile figo kufanya kazi yake vyema.


Unapokunywa maji kabla ya kula chochote asubuhi utauwezesha mwili wako pia kujenga misuli na kuzalisha seli mpya za damu.


2. Huboresha metabolim

Metaboli ni mchakato ambao mwilli hutumia vyakula (wanga, protini na mafuta) ili kupata nguvu na kujijenga. Hivyo basi, unywaji wa maji huwezesha mchakato huu kwenda vyema na kuufanya mwili kuwa na afya njema.


Kunywa maji kabla ya kula chochote unapoamka huufanya utumbo kuwa tayari kufyonza virutubisho. Kumbuka, maji ni muhimu kwa ajili ya watoto na watu wazima pia.


3. Husaidia kupunguza uzito


Wapo watu wanaopenda kupunguza uzito wa miili yao kwani uzito mkubwa si jambo zuri kiafya. Yakupasa kukumbuka kuwa unapoamka na kuanza kutumia vinywaji kama vile soda na juisi (sharubati) vitachangia sana kuongeza uzito wako wa mwili.


Utafiti unaonyesha kuwa soda ina sukari gramu 35 na gramu 140 za kalori ikilinganisha na maji ambayo vyote ni sifuri. Hivyo basi, ni vyema ukapendelea kunywa maji zaidi kuliko vinywaji vingine.


4. Huondoa kiungulia na matatizo ya umeng’enyaji wa chakula


Kunywa maji kutakusaidia kuzimua asidi inayopatikana tumboni ambayo ndiyo hupelekea tatizo la kiungulia. Sanjari na hayo unywaji wa maji utarahisisha na kuhimiza mchakato mzima wa umeng’enywaji wa chakula.


Hivyo basi, kama unakabiliwa na matatizo haya ni vyema kuzingatia unywaji wa maji kabla ya kutumia dawa mbalimbali.


5. Huboresha na kuimarisha ngozi


Utafiti unaonyesha kuwa kunywa maji takriban mililita 500 kunarahisisha mzunguko mzuri wa damu katika ngozi. Hivyo basi, hili hupelekea kuondoa sumu mbalimbali katika ngozi na kuiacha ngozi yako katika hali nzuri kiafya.

Cc:@_afyazone 




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!