Ticker

6/recent/ticker-posts

FAIDA ZA ULAJI WA MBOGA ZA NJEGERE MWILINI



 NJEGERE

• • • • •

FAIDA ZA ULAJI WA MBOGA ZA NJEGERE MWILINI


Bila shaka wewe sio mgeni kuhusu mboga hii ya njegere na hata kama hujawahi kuila basi umeiyona au kuisikia mahali flani.


Kuna faida nyingi kwa mtu ambaye anapenda kula mboga ya njegere katika swala zima la afya ya mwili, na katika makala hii tumechambua baadhi ya Faida za njegere mwilini.


FAIDA ZA ULAJI WA MBOGA ZA NJEGERE MWILINI NI PAMOJA NA;


✓ Njegere zina kiwango kizuri cha madini mbali mbali kama vile; madini ya chuma,madini ya magnessium,madini ya Phosphorus ambayo ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha mifupa,kinga ya mwili,uzalishaji wa damu n.k


✓ Ujali wa njegere pia husaidia kuupa mwili nguvu ya kutosha kutakana na kuwepo kwa kiwango kizuri cha wanga au carbohydrates


✓ Njegere ni chanzo kizuri sana cha protein mwilini ambayo husaidia sana katika matumizi mbali mbali mwilini kama vile; Kurepair seli za mwili, kuimarisha misuli,vichocheo vya mwili n.k


✓ Njegere pia huzalisha aina mbali mbali za vitamins mwilini Mfano; Vitamin A, Vitamin K n.k


✓ Njegere husaidia kudhibiti kiwango cha sukari mwilini hivo kusaidia sana kumkinga mtu na ugonjwa wa kisukari


✓ Njegere husaidia kumkinga mtu na magonjwa mbali mbali ya moyo, Saratani n.k


✓ Pia njegere husaidia kuimarisha mfumo mzima wa umeng'enyaji wa chakula mwilini


Hivo kula njegere kwa wingi kwa ajili ya Kuimarisha afya yako 


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments