Ticker

6/recent/ticker-posts

JINSI YA KUSAFISHA KITOVU CHAKO(kitovu kinaweza kuwa chanzo cha magonjwa)



KITOVU

• • • •

JINSI YA KUSAFISHA KITOVU CHAKO(kitovu kinaweza kuwa chanzo cha magonjwa)


Bila shaka wewe ni shahidi kwamba ukiangalia vizuri kitovu kama hujakisafisha vizuri utaona kuna mabaki ya uchafu yapo pale.


Mabaki yale huweza kutengeneza mazingira mazuri ya bacteria mbali mbali kuanza kuzaliana.


FAHAMU HII; Kuna utafiti ulifanyika mwaka 2012 kutoka kwa wataalam mbali mbali wa afya, ukaonyesha kwamba kuna wastani wa aina 67 za bacteria ambao huweza kupatikana kwenye kitovu chako bila wewe kujua.


Watu wengi wakishaoga husafisha mwili mzima bila kujali kitovu kipo safi au kipoje, lakini nikukumbushe kwamba usafi wa kitovu ni muhimu sana kuliko unavyofikiria.


Unaweza kuanza kuchunguza kitovu chako sasa na endapo ukaona kuna uchafu basi tumia njia hii hapa kujisafisha.


JINSI YA KUSAFISHA KITOVU CHAKO


Vifaa;


1. Unatakiwa uwe na Dettol


2. Unatakiwa uwe na kibeseni kidogo ambacho kina maji yaliyochanganywa na dettol


3. Unatakiwa uwe na kibeseni kingine cha maji safi


4. Unahitajika uwe na vipisi 3 vya pamba au kitambaa kidogo sana kisafi ambacho huweza kupenya vizuri kwenye kitovu chako kisha fanya yafuatayo;


✓ Weka kipisi cha kwanza cha pamba au kitambaa kidogo kisafi kwenye maji yaliyochanganywa na dettol kisha safisha kwa kuingiza ndani na kuzungusha ndani ya kitovu taratibu ili kuhakikisha unatoa uchafu wote nje, baada ya uchafu kutoka


✓ Chukua kipisi cha pili cha pamba au kitambaa safi kiweke kwenye maji masafi ambayo hayajawekwa chochote kisha tumia njia kama ya mwanzoni ya kuingiza ndani ya kitovu pamoja na kuzungusha vizuri taratibu


✓ Kisha malizia kwa kuchukua kipisi cha mwisho cha pamba au kitambaa kidgo safi ambacho ni kikavu pitisha tena kwa kuingiza ndani na kuzungusha tararibu vizuri.


Mpaka hapo kitovu chako kitakuwa safi, baada ya hapo kuwa muangalifu na kujali kitovu chako kila mara unaposafisha mwili wako.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments