Ticker

6/recent/ticker-posts

MADHARA YA KUCHORA TATTOO MWILINI



 TATTOO

• • • • •

MADHARA YA KUCHORA TATTOO MWILINI


Kwa hivi sasa swala la kuchora tattoo katika maeneo mbali mbali ya mwili ni fashion sana ambayo usipofanya hivo hasa kwa wasanii mbali mbali wa muziki unaonekana bado upo nyuma.


Lakini je tattoo unaweza kukusababishia madhara gani katika mwili wako? soma makala hii


MADHARA YA KUCHORA TATTOO MWILINI NI PAMOJA NA;


- Kuwa katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutokana na vifaa vyenye ncha kali kama sindano ambavyo huweza kutumika wakati wa kuchora tattoo mwilini


- Mtu kuwa katika hatari ya kupata tatizo la homa ya Ini au kwa kitaalam hujulikana kama Hepatitis B


- Mtu kuwa katika hatari ya kupata saratani ya ngozi kutokana na vitu kama Wino ambao huweza kuwa na kemikali ndani yake ambazo sio rafiki kwa ngozi wakati wa kuchora tattoo


- Kuanza kupata tatizo la mzio kwenye ngozi au wengine husema allergy ya ngozi


- Kuwa na makovu kwenye ngozi yako ya mwili


- Kuwa katika hatari ya kupata magonjwa mbali mbali ya ngozi


- Kukosa nafasi mbali mbali za kazi katika sekta au maeneo mbali mbali Mfano; jeshini hawaruhusu kabsa mtu kuchora tattoo mwilini


- Mtu kuwa katika hatari ya kupata tatizo la damu kuvuja na kuganda kwenye ngozi


- Mtu kupata shida ya kufanya vipimo mbali mbali wakati anaumwa


- Kuwa katika hatari ya kuvuja damu bila kuganda kwa mtu ambaye ana tatizo la damu kutokuganda au yule anayetumia dawa kwa ajili ya damu isigande.


Hivo kwa maana nyingine namaanisha ni hatari kwa mtu ambaye anatatizo la damu kutokuganda, lakini pia ni hatari kwa mtu ambaye ana tatizo la damu kuganda yenyewe halafu anatumia dawa ili damu isigande 

n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments