Ticker

6/recent/ticker-posts

MADHARA YA MATUMIZI YA UGORO(tumbaku)



UGORO

• • • •

MADHARA YA MATUMIZI YA UGORO(tumbaku)


Ugoro ni tumbaku ambayo imesagwa ikawa katika mfumo wa unga na kuanza kutumiwa na watu mbali mbali ambapo wengine hunusisha puani na wengine huilamba pia.


Wapo watu wengi bado wanatumia ugoro, watu wazima na hata vijana wadogo pia, bila kufahamu kwamba matumizi ya vitu hivi yana athari kubwa kwa afya zao.


Wengine husema wanapenda kutumia ugoro maana hulewesha haraka kama vile pombe,


Hata hivo mtumiaji huweza kuona madhara mengi baada ya kutumia ugoro kwa muda wa kuanzia miaka mitano,kumi na kuendelea.


Matumizi ya Sigara, Ugoro au madawa ya kulevyia mengine ni hatari kwa afya yako, epuka vitu hivi kwani madhara yake ni mengi kuliko faida.


Ndani ya Ugoro kuna kemikali kama Vile; Nitrosamines na Nicotine ambazo ndyo kisababishi kikubwa cha Saratani kwenye mwili wa mtumiaji


MADHARA YA MATUMIZI YA UGORO


- Moja ya madhara ya kutumia Ugoro ni mtumiaji kuwa katika hatari ya kupata Saratani ya Kinywa


- Mtumiaji kupata magonjwa kwenye mfumo wake wa hewa


- Mtumiaji Kupata Saratani ya tumbo


Mtumiaji Kupata Saratani ya ulimi


- Mtumiaji Kupata Saratani ya kongosho


- Mtumiaji Kupata Saratani ya koromeo n.k


- Vile vile mtumiaji huweza kupata madhara mengine kama vile; 


• Meno ya mbele kung'oka


• Meno kulegea sana


• Kupata matatizo ya Fizi


• Meno kubadilika rangi 


• Kuchubuka mdomo


• Kutoa harufu mbaya mdomoni

n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.








Post a Comment

0 Comments