Ticker

6/recent/ticker-posts

UGONJWA WA KIBOFU CHA NYONGO(chanzo,dalili na Tiba)



 KIBOFU CHA NYONGO

• • • • •

UGONJWA WA KIBOFU CHA NYONGO(chanzo,dalili na Tiba)


Ugonjwa wa kibofu cha nyongo ni mjumuisho wa magonjwa yote ambayo hushambulia kifuko cha nyongo na kusababisha madhara mbali mbali kama vile; Kifuko cha nyongo kuvimba, kifucho cha nyongo kuziba,kifuko cha nyongo kupasuka au kuwepo kwa mawe kwenye kifuko cha nyongo.


Mfano wa magonjwa kwenye kifuko cha nyongo ni pamoja na;


1. Ugonjwa wa kuwa na mawe kwenye kifuko cha nyongo ambao kwa kitaalam hujulikana kama Gallstones


2. Ugonjwa wa kuvimba kwa kifuko cha nyongo ambao hujulikana kama Cholecystitis


3. Ugonjwa wa majipu ndani ya kifuko cha nyongo yaani Gallbladder  abscesses


4. Tatizo la Kansa ya kifuko cha nyongo

N.k


CHANZO CHA UGONJWA WA KIBOFU CHA NYONGO


• Uwepo wa kiwango kikubwa cha Cholestrol kwenye nyongo


• Tatizo la Kansa


• Matumizi ya vitu vyenye kiwango kikubwa cha Sumu mwilini kama vile; dawa,pombe n.k


• Mashambulizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile; Bacteria, Virusi N.k


DALILI ZA UGONJWA WA KIBOFU CHA NYONGO NI PAMOJA NA;


- Mgonjwa kupata maumivu makali juu kidogo ya kitovu upande wa kulia kuelekea mgongoni


- Mgonjwa kupata maumivu wakati wa kupumua


- Mgonjwa kupata hali ya kichefuchefu pamoja na kutapika


- Mgonjwa kupata maumivu ya tumbo mara kwa mara


- Mgonjwa kupata tatizo la kuharisha


- Mgonjwa kupata shida ya Tumbo Kujaa gesi


- Ngozi,macho,au viganja vya mikono kubadilika rangi na kuwa manjano


- Joto la mwili kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa


- Mgonjwa kukojoa mkojo wenye rangi nyeusi


MATIBABU YA UGONJWA WA KIBOFU CHA NYONGO


-Matibabu ya magonjwa haya huhusisha njia mbali mbali ikiwa ni pamoja na matumizi ya dawa na Huduma ya upasuaji kwa Mgonjwa ambayo huhusisha kuondoa kabsa au kurekebisha kifuko hiki cha Nyongo.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments