Ticker

6/recent/ticker-posts

UGONJWA WA KULEGEA KWA MISULI YA MWILI(myasthenia gravis)



MISULI

• • • • •

UGONJWA WA KULEGEA KWA MISULI YA MWILI(myasthenia gravis)


Myasthenia Gravis ni ugonjwa ambao huhusisha kulegea pamoja na kuchoka kwa misuli mbali mbali ya mwili ambayo ipo chini ya uthibiti wako.


Misuli hyo ni kama vile; misuli ya macho, misuli ya miguu, misuli ya mikono,misuli ya shingoni,misuli ya usoni n.k


CHANZO CHA UGONJWA HUU


- Tatizo ambalo hutokea kwenye mfumo wa Nerves za mwilini


- Tatizo la mfumo wa kinga ya mwili


- Matumizi ya baadhi ya dawa ambazo huathiri moja kwa moja misuli ya mwili


DALILI ZA UGONJWA HUU NI PAMOJA NA;


- Mtu kushindwa kufungua vizuri jicho moja kutokana na misuli ya jicho hilo kulegea


- Mtu kuona marue rue kutokana na misuli ya macho kulegea


- Mtu kushindwa kumeza kitu vizuri kutokana na misuli ya kooni na shingoni kutokufanya kazi vizuri


- Mtu kushindwa kuongea kutokana na misuli ya kinywani kulegea sana


- Mtu kubadilika usoni na kuonekana anacheka wakati hacheki kutokana na misuli ya usoni kulegea


- Mtu kushindwa kabsa kutafuna chakula mdomoni kutokana na misuli kulegea


- Na dalili zingine kama vile;


✓ Kupata shida ya upumuaji


✓ Kushindwa kutembea kabsa

n.k


MATIBABU YA UGONJWA HUU


• Zipo dawa mbali mbali ambazo hutumika kama vile; Prednisone(Cortosteroids) pamoja na dawa zingine jamii ya Immunosuppresants


Japo lazima matibabu yatokane na chanzo cha tatizo


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments