Ticker

6/recent/ticker-posts

ULAJI WA BAADHI YA VYAKULA HUONGEZA UWEZAKANO WA MTU KUPATA KANSA



KANSA

• • • • •

ULAJI WA BAADHI YA VYAKULA HUONGEZA UWEZAKANO WA MTU KUPATA KANSA


Tafiti mbali mbali za wataalam wa afya na magonjwa ya binadamu zinaonyesha kwamba moja ya vitu ambavyo huongeza uwezekano wa mtu kupata kansa ni pamoja na kile anachokula.


Huku vyakula mbali mbali kama vile; nyama nyekundu au vyakula vya mafuta sana,watu wakishauriwa kuepukana navyo ili kujikinga na hatari ya kupata magonjwa kama kansa na magonjwa mbali mbali ya Moyo.


Kutokufanya mazoezi, kula vyakula ambavyo ni Processed Foods, pamoja na kiwango kikubwa cha sukari ni hatari kwa afya yako,


Ulaji wa sukari kwa kiwango kikubwa huchochea uzalishaji wa  kiwango kikubwa cha Kichocheo cha Insulini, hali ambayo hupelekea hatari ya ukuaji wa seli kuliko kawaida na mtu kuwa katika hatari ya kupata tatizo la Kansa.


Baadhi ya kansa hizo ni pamoja na;


1. Kansa ya kwenye mdomo


2. Kansa ya Ini


3. Kansa ya kizazi au Uterine cancer


4. Kansa ya tumbo


5. Kansa ya Figo


6. Na kansa ya matiti kwa wanawake ambao wamefikia ukomo wa hedhi


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments