Chanzo cha Maambukizi kwenye Sikio(Acute Otitis media),DALILI NA TIBA

 SIKIO

• • • • •

Chanzo cha Maambukizi kwenye Sikio(Acute Otitis media),DALILI NA TIBA


Acute Otitis media, ni maambukizi ambayo hutokea sehemu ya ndani ya Sikio yaani Middle Ear, maambukizi haya huwapata watoto zaidi ya watu wazima


CHANZO CHA MAAMBUKIZI KWENYE SIKIO


• Tatizo hili husababishwa na vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile BACTERIA au VIRUSI, japo pia kuna baadhi ya sababu huongeza uwezekano wa mtu kupata tatizo hili, na sababu hizo ni kama vile;


✓ Allergy


✓ Tatizo la mafua


✓ Maambukizi yaani Sinus infection


✓ Uvutaji wa Sigara

n.k


DALILI ZA MAAMBUKIZI KWENYE SIKIO


1. KWA WATOTO


- Mtoto kupata maumivu makali ya sikio hasa wakati akijaribu kulala


- Sikio kutoa maji maji,usaha au damu


- Mtoto kupata shida ya kukosa usingizi


- Mtoto kulia sana


- Mtoto kupata Maumivu makali ya kichwa


- Mtoto kupata tatizo la kutokusikia vizuri


- Joto la mwili kuwa juu au mtoto kuwa na Homa


- Kupoteza balance ya mwili


- Kukosa hamu ya kula chakula


- Mtoto kupata Maumivu makali ya shingo


- Mtoto kuhisi sikio kujaa na kuwa zito


- Mtoto kutapika na kuharisha

n.k


2. KWA WATU WAZIMA


- Kupata maumivu makali ya sikio


- Sikio kuvuja maji maji,usaha au Damu


- Kupata tatizo la kutokusikia vizuri

n.k


MATIBABU YA TATIZO HILI


- matibabu ya tatizo hili huhusisha dawa mbali mbali kama vile; Dawa jamii ya antibiotics, dawa za maumivu n.k, 


kulingana na chanzo chake, hivo ni vizuri mgonjwa kwenda hospital na kuchunguzwa vizuri kabla ya kuanza tiba



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!