Ticker

6/recent/ticker-posts

CHANZO CHA MAUMIVU YA KITOVU AU KITOVU KUVUTA WAKATI WA UJAUZITO



 KITOVU

• • • • • •

CHANZO CHA MAUMIVU YA KITOVU AU KITOVU KUVUTA WAKATI WA UJAUZITO


Kuna baadhi ya wanawake wakiwa wajawazito husema wanapata maumivu kwenye kitovu, na wengine husema kitovu kinavuta,


je chanzo chake ni nini? je ni tatizo au hali ya kawaida? soma kujua


Maumivu ya kitovu au kitovu kuvuta wakati wa ujauzito hutokana na ukuaji wa mtoto, kadri mtoto anavyokuwa ndivo husababisha presha kubwa,mgandamizo,ngozi kuvutika na tumbo kutanuka,


Baadhi ya wanawake hupata maumivu ya kitovu kwenye hatua za mwanzoni za ukuaji wa mimba, na wengine hupatwa sana na hali hii kwenye wiki za mwishoni za ujauzito,


Unashauriwa kulala ubavu hasa hasa ubavu wako wa kushoto, tabia hii ya kulala ubavu hupunguza sana na kwa kiasi kikubwa tatizo hili.


ANGALIZO; endapo unapata maumivu makali ya kitovu huku yakiambatana pamoja na shida hizi hapa chini, nenda hospital;


- Maumivu ya kitovu ambayo huambatana na damu kuvuja ukeni


- Maumivu ya kitovu ambayo huambatana na kitovu kuvimba


- Maumivu ya kitovu ambayo huambatana na joto la mwili kuwa juu(homa)


- Maumivu ya kitovu ambayo huambatana na  kutapika sana


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments