UDONGO
• • • • •
CHANZO CHA TATIZO LA KULA UDONGO NA MADHARA YAKE
Tatizo la kula udongo ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Geophagy ni tatizo ambalo hutokana na upungufu wa madini ya chuma mwilini.
Tatizo hili huweza kutokea kwa mtu yeyote japo kwa asilimia kubwa limeonekana kwa wakina mama wajawazito.
KWANINI WAKINA MAMA WAJAWAZITO HUPENDA KULA UDONGO?
- Mbali na shida ya upungufu wa madini ya chuma mwilini,wakina mama wengi hupenda kula udongo wakiwa wajawazito kwani huaminu kwamba udongo huwasaidia katika;
• Kuondoa au kupunguza hali ya kichefuchefu
• Kuleta hamu ya kula
• Kupunguza uchovu
n.k
MADHARA YA KULA UDONGO
madhara ya kula udongo kwa asilimia kubwa hutegemea na chanzo au sehemu ambapo udongo huo umetoka
- Udongo huweza kubeba uchafu wa kila aina kama vile kinyesi,mikojo n.k hali ambayo huweza kumsababishia mlaji magonjwa mbali mbali kama vile; Homa ya matumbo au Typhoid n.k
- Mtu huweza kuanza kupata tatizo la tumbo kuuma sana
- Mtu kupata tatizo la kuanza kuharisha baada ya kula udongo
- Lakini pia udongo huweza kubeba viambata vyenye sumu kali ambavyo ni hatari mwilini
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!