PUA
• • • • •
CHANZO CHA TATIZO LA KUTOA HARUFU MBAYA PUANI
Tatizo la kutoa harufu mbaya puani huweza kutokea kwa mtu yoyote, lakini kwa bahati nzuri ni kwamba tatizo hili haliwezi kuwa la muda mrefu sana au la kudumu, kwa asilimia kubwa ya watu wenye tatizo hili huisha ndani ya muda mfupi
Tatizo hili huweza kusababishwa na sababu mbali mbali,
CHANZO CHA TATIZO LA KUTOA HARUFU MBAYA PUANI
- Mtu kupatwa na mashambulizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile; fangasi,virusi au Bacteria
- Mtu Kupatwa na tatizo la kuota vinyama puani hali ambayo hujulikana kwa kitaalam kama Nasal polyps
- Kuanza kutoa harufu puani baada ya kutolewa mpira wa puani ambao ulitumika kwa sababu mbali mbali kama vile; kwa ajili ya kupata chakula, Hewa n.k
- Kupatwa na tatizo la jino au meno kuharibika na sehemu ya jino kuoza kutokana na mashambulizi ya wadudu kama Bacteria n.k, hali ambayo husababisha harufu mbaya kutokea puani
- Kuwa na tatizo la figo kwa muda mrefu yaani Chronic kidney diseases, hali ambayo hupelekea kukusanyika kwa kiwango kikubwa cha taka mwili, na kuleta athari hadi puani
n.k
MATIBABU YA TATIZO HILI LA KUTOA HARUFU MBAYA PUANI
Tatizo hili hutibika kabsa kulingana na chanzo chake,hivo kutana na wataalam wa afya kwa ajili ya vipimo na matibabu zaidi
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!