CHANZO CHA TATIZO LA MOYO KUTANUKA na Kuwa Mkubwa,DALILI NA MATIBABU YAKE
MOYO
• • • • • •
CHANZO CHA TATIZO LA MOYO KUTANUKA,DALILI NA MATIBABU YAKE
Tatizo la moyo kutanuka huathiri kwa kiasi kikubwa utendaji kazi wa moyo,ikiwa ni pamoja na usukumaji wa damu katika maeneo mbali mbali mwilini,
CHANZO CHA TATIZO LA MOYO KUTANUKA
Hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo huhusishwa na tatizo la moyo kutanuka, japo zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia mtu kuwa na tatizo la moyo kutanuka, na miongoni mwa sababu hizo ni kama vile;
✓ Kuwepo kwa ukinzani mkubwa wakati wa damu kuingia na kutoka kwenye moyo
✓ Kuwa na magonjwa mbali mbali ya moyo kama vile; Mishipa ya damu ndani ya moyo kuwa myembamba sana au kuziba hali ambayo husababisha moyo kutumia nguvu ya ziada kusukuma damu,
✓ Kuwa katika familia ambayo kuna mtu mwenye tatizo hili
✓ Kuwa na tatizo la shinikizo la damu au Presha
✓ Hitilafu kwenye moyo toka unazaliwa
✓ Kuna baadhi ya wakina mama hupatwa na tatizo la moyo kutanuka kwa muda mfupi kipindi cha ujauzito na baadae kuisha
✓ Mtu kupatwa na tatizo lolote ambalo husababisha misuli ya moyo ikose nguvu
✓ Kuwa na tatizo la mapigo ya moyo kwenda mbio
✓ Mabadiliko ya vichocheo mwilini
n.k
DALILI ZA TATIZO LA MOYO KUTANUKA NI PAMOJA NA;
Hakuna dalili za moja kwa moja za tatizo hili ila kuna dalili jumuishi ambazo hata mtu mwenye matatizo mengine yamoyo huweza kupata, dalili hizo ni kama vile;
- Mtu kupata uvimbe kwenye maeneo mbali mbali kama vile miguuni
- Mtu kupata shida ya upumuaji
✓ Viungo mbali mbali kama vile vidole kufa ganzi
✓ Mwili kuishiwa na nguvu kabsa
✓ Kupatwa na hali ya kizunguzungu
✓ Kupata maumivu ya kifua
✓ Kupata maumivu makali ya kichwa
✓ Mtu kupoteza fahamu
✓ mtu kuwa katika hatari ya kupooza au kuparalyze
n.k
MATIBABU YA TATIZO LA MOYO KUTANUKA
- Matibabu ya tatizo hili huhusisha matumizi ya dawa mbali mbali pamoja na huduma ya upasuaji wa moyo.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!